January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Mkuu Mstaafu Majaliwa awajulia hali mzee King Kiki, Mkuu wa Wilaya ya Mlele

WAZIRI Mkuu Mstaafu Kassim Majaliwa amemtembelea na kumjulia hali mwanamziki mkongwe nchini Kikumbi Mwanza Mpango maarufu kama King Kikii, Nyumbani kwake Temeke kwa Azizi Ally, Jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu Mstaafu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Msanii mkongwe wa muziki wa dansi Kikumbi Mwanza Mpango, maarufu kama (King Kiki) , wakati alipomjulia hali msanii huyo anayesumbuliwa na matatizo ya pingiri za mgongo, nyumbani kwake Temeke kwa Azizi Ali.

Majaliwa alimpa pole Kinkii anayesumbuliwa na matatizo ya mgongo na amemtakia pona ya haraka ili aweze kuendelea na majukumu yake kama kawaida.

Aidha,Majaliwa pia alimjulia hali Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rechal Kasanda ambaye amelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari Wilayani Mlele, Mkoani Katavi alipokuwa kwenye ziara ya kikazi.

Waziri Mkuu Mstaafu, Kassim Majaliwa akimjulia hali Msanii mkongwe wa muziki wa dansi Kikumbi Mwanza Mpango, maarufu kama (King Kiki) , anayesumbuliwa na matatizo ya pingiri za mgongo, nyumbani kwake Temeke kwa Azizi Ali.

Akizungumza na Kasanda, Majaliwa alimtakia pona ya haraka ili aendelee na majukumu yake ya kuwatumikia WanaKatavi.

Waziri Mkuu Mstaafu, Kassim Majaliwa, akimpa pole Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Rechal Kasanda ambaye amelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari Wilayani Mlele, Mkoani Katavi alipokuwa kwenye ziara ya kikazi. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera.