Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye bonanza maalumu la waandishi wa habari na wafanyakazi wa vyombo vya habari nchini “TASWA Media Day Bonanza 2024” litakalofanyika Februari 10, mwaka huu, Msasani Beach Club, Dar es Salaam.
Katika tukio hilo linalotarajiwa kuanza saa 3:00 asubuhi, litahusisha pia uzinduzi wa Tuzo za Wanamichezo Bora wa Tanzania mwaka 2024, zinazotolewa na TASWA.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TASWA, jana tukio hilo litahusisha mchezo wa riadha, mpira wa miguu, mpira wa kikapu, mpira wa wavu, kushindana kunywa soda, kushindana kufukuza kuku na kushindana kula ugali na kuku mzima wa kuchoma.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania