Na Mwandishi Wetu,TimesmajiraOnline,Dar
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia,
Dkt. Abiy Ahmed Ali amewasili nchini jana kuanza ziara yake ya kitaifa ya siku tatu.
Amewasili nchini jana na kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba.
Dkt. Abiy amepokelewa rasmi na mwenyeji wake Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Pamoja na mambo mengine ziara ya Waziri Mkuu Abiy inalenga kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Ethiopia katika maeneo ya kimkakati ikiwemo usafirishaji kwa njia ya anga, nishati, kilimo na mifugo, biashara na uwekezaji na Ushirikiano katika sekta za elimu, uhamiaji, na ulinzi na usalama
Ziara hiyo ambayo itakamilika kesho inafanyika kufuatia
mwaliko wa Rais Samia.

More Stories
REA yaing’arisha Nishati Safi EXPO 2026 Dar
Wananchi watahadharishwa dhidi ya bidhaa bandia
RAS apongeza mfumo kudhibiti upotevu wa mafuta