Na Mwandishi wetu,Timesmajira,Online
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.
Mradi huo unatekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa kusimamiwa na Mshauri Elekezi, Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), kwa gharama ya shilingi bilioni 2.2 chini ya Mradi wa Kukuza Elimu na Ujuzi kwa Kazi zenye Tija (ESPJ).
Chuo hicho ambacho kinatarajia kukamilika mwezi Disemba 2021, kitakuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi 560 kwa mwaka katika fani za ufundi umeme, Useremala, Uungaji na Uchomeleaji vyuma, Uashi, Ushonaji na Mitindo ya Mavazi, Usindikaji Vyakula na Tehama .
More Stories
Rais Mwinyi aipongeza Kampuni ya Yas kushirikiana na ZHC
Raha ya WiFi za bure na mtego kwa taarifa zako za siri
Mke wa Rais wa Finland atembelea Makumbusho ya Taifa