Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 07, 2024 ameendelea na ziara mkoani Iringa ambapo ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule ya Sekondari ya wasichana ya Iramba iliyopo katika kijiji cha Iramba, kata ya Itandula kwenye Halmashauri ya Wilaya Mufindi.
Akizungumza baada ya kufanya ukaguzi wa shule hiyo Mheshiwa Majaliwa ameitaka Halmashauri hiyo kuendelea kubaini vyanzo vitakavyoongeza fedha ili waweze kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo. “Ninawapongeza madiwani kwa wazo la kutenga fedha na kujenga mradi huu wa shule”
“Moja kati ya mapungufu ya baadhi ya halmshauri ni kutotumia fedha za ndani kujenga miradi inayoonekana, ujenzi wa shule hii ni mfano wa kuigwa na halmashauri zote, ongezeni kasi ya mkamilishe mradi huu kwa wakati”
Pia Mheshimiwa Majaliwa amewataka kutumia fedha iliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo ili miundombinu yote itakayojengwa iendane na fedha iliyotolewa.
Katika hatua nyingine Mheshimiwa Majaliwa ameagiza kupitiwa kwa gharama za ujenzi wa nyumba za walimu kupitia kamati ya elimu ya halmashauri “Fanyeni mapitio ya fedha mliyopanga kutumia kwa ajili ya nyumba za walimu, shilingi milioni 100 ni nyingi kwa nyumba moja”
Pia ameagiza kuondolewa na kurudishwa kwa fundi madawati yote ambayo hayana eneo la kuweka daftari kwa ajili ya wanafunzi.
Ujenzi wa Shule hiyo unategemewa kugharimu kiasi cha Bilioni 1.78 mpaka kukamilika kwake, ukihusisha jengo la utawala (1) Madarasa (8) Ofisi (4), Maabara (1), Chumba cha TEHAMA (1) Nyumba za walimu (5), Bwalo la chakula (1) na Mabweni (4).
Mpaka sasa kiasi cha shilingi milioni 363.8 kimepokelewa ikiwa ni shilingi milioni 2.2 nguvu za wananchi na Halmashauri ya wilaya shilingi milioni 361.6.
Kwasasa shule hiyo ina jumla ya madarasa 8, Ofisi 4 na bweni lenye uwezo wa kulaza wanafunzi 80 lipo katika hatua ya kuwekwa marumaru.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato