January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Mkuu aahidi kutatua changamoto zinazozikabili vyombo vya habari nchini

Ashura Kazinja na Severin Blasio,TimesMajira online,Morogoro

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa amesema kuwa yapo madeni mengi ambayo vyombvo vya habari vinadai taasisi nyingi za Serikali ambapo hawana budi kulipa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa akizungumza kwenye mkutano hu

Waziri Mkuu hayo leo mkoani Morogoro kwenye Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF) alisema kuwa ifike mahali wanaodaiwa waweze kuvilipa vyombo vya habari ili navyo viweze kujiendesha katika mambo yake mbalimbali.

Aidha amevitaka vyombo vya habari nchini kutumia kalamu zao kutangaza vituo vya utalii vilivyopo ili kusaidia nchi kupata fedha za kigeni na hivyo kuongeza pato la Taifa.

‘’Tumieni nafasi zenu, kalamu zenu kuhakikisha mnatangaza utalii wa nchi yetu…yapo mataifa yanatumia kalamu zao kutanngaza vivutio vya nchi yao na huku sisi tukibaki tumenyamaza’’amesema Majaliwa.

Amesema kuwa Serikali ipo tayari kushirikiana na vyombo vya habari katika kupanga mikakati,mipango na sera ya Taifa ya maendeleo ya nchi yetu ili kuhakikisha vyombo vinatimiza wajibu wake ipasavyo.

Hata hivyo Majaliwa alitoa agizo kwa waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo kuandaa mpango maalum wa kuunda bodi ya ithibati kwa ajili ya kuandaa baraza huru la wanahabari litakalosaidia kuwasilisha mipango yao.

Amesema Jukwaa la Wahariri ni chombo huru na pia linatakiwa huru hivyo Serikali inaendelea kupokea maoni ya kuangalia namna ya kuboresha sheria zilizopo na kuendelea kufanya vyombo vya habari kuwa huru.

Waziri Mkuu Kassim Majaliea akizungumza na katibu wa TEFNevile Meena

Awali Akizungumza Makamu mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Deodatus Balile amesema kuwa vyombo vingi vya habari vimeshuka kiuchumi kutokana na kutolipwa madeni ya matangazo.

Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari nchini wakimsikiliza waziri Mkuu

Balile ameiomba Serikali kuona umuhimu wa kurejesha matangazo ya Bunge moja kwa moja pamoja kuondoa sheria kandamizi zinazobana uhuru wa habari .

Amesema kuwa kuna umkuhimu ea serikali kufanya marekebisho ya sheria ya habari hususani kwenye vipengele vinavyobana uhuru wa vyombo vya habari.

Kwa habari zaidi soma gazeti la Majira kesho