January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Makamba akutana na mwakilishi wa kikundi cha Kusama Wilayani Musoma

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba akizungumza na mwakilishi wa kikundi cha Kusama, wilayani Musoma. Kikundi hicho cha wakina mama kinafanya kazi za kukaanga dagaa kwa kutumia nishati ya kuni na mkaa.

Aidha Mhe. Makamba aliwaelimisha wanakikundi hao madhara ya kiafya na kimazingira ya muda mrefu ya kutumia kuni na mkaa. Kwa Mkoa wa Mara, watu kati ya 400- 600 kwa mwaka huugua kutokana na athari za Moshi wa kuni na mkaa. Mhe Makamba amewaahidi wana kikundi hao kufunga mfumo wa gesi ya kupikia ili wafanye shughuli hizo kwa kutumia nishati safi.