Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dr. Ashatu Kijaji amewataka wananchi wa mkoani Morogoro na watanzania wote kwa ujumla kuchangamkia fursa za mikopo zinazotolewa na Mfuko wa SELF Ili kujiinua kiuchumi na kuchangia pato la Taifa.
Waziri Kijaji ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akikabidhidhi hundi ya shilingi Milioni 700 kwa Mkurugenzi wa Builders Financial Services: Damasi Masawe ili aweze kuwakopesha watanzania wajasiriamali wadowadogo waliopo sehemu mbalimbali za Morogoro, Chalinze na Mlandizi pia alikabidhi hundi ya kiasi cha shilingi milioni 120 kwa kampuni ya Star Natural Ltd. Hundi hizo zilitolewa na Mfuko wa SELF wenye makao yake makuu jijini Dar es salaam.
Waziri Kijaji aliongea hayo wakati akifunga maonesho ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji wananchi kiuchumi yaliyofanyika kitaifa katika uwanja wa Jamhuri Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro mkoani humo.
Dr. Kijaji amebahanisha kuwa serikali kwa kwa kupitia Mfuko wake wa SELF zinafanya jitihada kubwa kusaidia na kuwezesha wananchi kushiriki katika shughuli za kiuchumi lakini ushiriki wa wananchi wenyewe umekuwa si wakuridhisha.
Naye Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Martine Shigela akiwakilisha salamu za mkoa amewataka wakazi wa mkoa huo kuwa kupitia vikao vya kiutendaji mkoa utatumia mikakati mbalimbali na kubainisha mifuko na programu za kuwasaidia wananchi kiuchumi kwa kuongeza, Uzalishaji hasa katika sekta ya kilimo na kukaribisha wawekezaji mkoani humo kwani ardhi ipo kubwa na yakutosha.
More Stories
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi
Lina PG Tour yafufua gofu Moshi
Kampeni ya Sako kwa Bako yawafikia Kanda ya Kati