February 20, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Kabudi atoa somo kwa BASATA

Na Bakari Lulela,Timesmajira

WITO umetolewa na wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo kwa kulitaka Baraza la sanaa BASATA kuhakikisha wanaandaa mifumo wezeshi ya Hamasi na Tausi iliyotolewa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassani iliyogharimu shilingi million 700 katika kuwasaidia wasanii kifikia lengo la kuendeleza shughuli mbalimbali za kisanii.

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni katika ukumbi wa Baraza hilo jijini Dar es salaam na waziri wa habari, utamaduni , sanaa na michezo palamagamba Kabudi amesema mifumo hiyo wezeshi itawasaidia wasanii wetu kukabiliana na changamoto mbalimbali ambazo ni adui wa maendeleo na kuweza kifikia malengo tarajiwa hususan masuala ya kiuchumi.

” Mifumo hiyo ni Suluhu ya changamoto kwa wasanii pia suala la maadili ni jambo muhimu katika kuendeleza na kuzipa ubora kazi zote za sanaa ambazo zinaheshimu utu na uhuru wa mtanzania hivyo Baraza la sanaa ni wawezeshaji na wasimamizi wa shughuli za kisanii kwa wasanii wote,” amesema Kabudi

Pamoja na hilo waziri Kabudi ameeleeza umuhimu mkubwa wa muziki wa nyimbo za singeli katika kudumisha utamaduni wa mtanzania ambapo ametaka upewe kipaumbele kwenye maeneo mbalimbali kisekta ndani na nje ya mipaka ya Tanzania .

Kwa upande wake mtendaji mkuu wa Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) Dkt.Kedmon Mapana amesema kuwa wataendelea kutekeleza maelezo yote yaliyotolewa na waziri Ili kuhakikisha maadili na muziki wa singeli vinakuwa ni alama katika kizazi chetu.

Aliendelea kusema kutekeleza mifumo saidizi ya Hamasi na Tausi inakuwa kipaumbele kwenye makundi ya wasanii Ili kudumisha azma ya kuendeleza sekta ya sanaa hapa nchini kwa wasanii wetu.

Mkuu huyo ameeleeza kupitia michoro ya tinga tinga wataendelea kuipa umuhimu mkubwa wasanii hao ambao michoro yao inaonyesha ishara tosha ya kazi Bora zinazovutia na kupendwa barani Afrika na ulimwenguni kote.