November 14, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Gwajima atoa cheti kwa Mwenyekiti Malagashimba

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Makundi Maalum Dorothy Ngwajima, ametoa cheti cha pongezi kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Amani Kata ya Kipunguni Jimbo la Ukonga Daniel Malagashimba kwa kutambua mchango wake katika kuisaidia Jamii katika masuala mbalimbali yakiwemo ya kuisaidia Serikali kupinga vitendo vya ukatili ambapo Mtaa wa Amani Kata ya Kipunguni kikundi Cha Sauti ya Jamii kimekuwa mfano Wilayani Ilala .

Waziri Dorothy Ngwajima alitoa cheti hicho cha pongezi leo wakati wa kuzindua Jengo la Sauti ya Jamii’ Kipunguni ambalo litakuwa linatoa Elimu Katika masuala ya kupinga ukatili kwa jamii ambapo Sauti ya Jamii’ Kipunguni imesaidia Serikali Tarafa ya Ukonga kupinga vitendo hivyo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Amani Daniel Malagashimba

“Siku ya Wanawake Duniani Machi 8 nilikuja Kata ya Kipunguni nilitoa ahadi nitarudi Mimi ni Waziri wa Mitaani ,Waziri wa Jamii’ kwangu ni Mitaani Mimi sio Waziri wa kusoma Makabrasha mfano kuna Taarifa za kufanyiwa Ukatili lazima utoke ofisini wende mtaani watoto wengine wanabakwa na ndugu Zao ” alisema Ngwajima

Alisema alipokuja siku ya Wanawake alipokewa katika Mtaa wa Amani katika Sauti ya Jamii’ amelizishwa na kazi zinazofanywa na kikundi hicho na Leo nampongeza Mwenyekiti Daniel Malagashimba kwa kusimamia vizuri Sauti ya Jamii’ kuweza kufikia
malengo yake mpaka Sasa kikundi hicho wanasonga mbele .

Waziri Ngwajima alisema amekuwa akifatilia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Samia Suluhu Hassan, ameunda Wizara hii Ili pia tuweze kusimamia majukwa ya uwezeshaji Wanawake Kiuchumi waweze kupata fursa mbali mbali nawaomba watendaji mfatilie mtaani msikae ofisini .

Alisema anatarajia kufanya ziara Katika Shule,hospitalini na Polisi kuangalia madawati ya jinsia yanavyoendeshwa katika masuala ya ukatili wa kijinsia .

Akizungumzia Sauti ya Jamii’ Kipunguni alisema ni kituo Cha mfano wa kuigwa napongeza Sauti ya Jamii’ Pamoja na Jimbo la Ukonga Sauti ya Jamii’ Kipunguni kitaleta Tija kwa kusaidia Jamii kutoa elimu ya ushonaji Pamoja na Kilimo .

Sauti ya Jamii’ kilichozinduliwa Leo kiwe chachu kwa maendeleo ametaka halmashauri kuiunga mkono Sauti ya Jamii’ kwa kazi zake wanazofanya.

Kwa upande wake Mwenyekiti Kamati Ujenzi wa Sauti ya Jamii’ Kipunguni Juma Rashid alisema Wana kikundi walikuwa wanaweka akiba kidogo kidogo na kufanya mafunzo mpaka wakapata fedha za kununua Kiwanja shilingi milioni 5 ujenzi wa Ofisi umegharimu shilingi milioni 6.9 jumla gharama zote za Ujenzi shilingi milioni 11.9 Jengo la Ofisi ina sehemu Mbili sehemu ya Ofisi na sehemu ya ushonaji .

Mkurugenzi wa Sauti ya Jamii’ Kipunguni Selemani Bishagazi alisema kituo Cha Sauti ya Jamii’ kitakuwa kinatoa Elimu mbalimbali ya kupinga vitendo vya Maswala ya ukatili pia kutakuwa na wanasheria katika kituo Cha Sauti ya Jamii’ .

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Amani Daniel Malagashimba akionesha cheti alichopewa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Makundi maalum Dorothy Ngwajima kushoto wakati akisakimiana na Mama Malagashimba Leo Octoba 19/2022 wakati wa kuzindua Jengo la Jamii Kipunguni katikati Diwani wa Kipunguni Steven Mushi
Waziri wa Maendeleo ya Jamii jinsia na Makundi Maalum Dkt.Dorothy Ngwajima akisakimia Wananchi wa Kipunguni Wilayani Ilala leo Octoba 19/2022 katika ziara yake Jimbo la Ukonga ambapo alizindua Jengo la Ofisi ya Sauti ya Jamii’ Kipunguni kulia anayesalimia ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Amani Daniel Malagashimba
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na MAKUNDI Maalum Dkt.Dorothy Ngwajima ,kulia mara baada kuzindua Jengo la Sauti ya Jamii’ Kipunguni Wilayani Ilala Leo Octoba 19/2022 kushoto Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Amani Daniel Malagashimba na Diwani wa Kipunguni Steven Mushi
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Arch,LUDIGIJA akizungumza na Wananchi wa Kipunguni Jimbo la Ukonga Leo wakati wa Uzinduzi wa jengo la Ofisi ya Sauti ya Jamii’ Kipunguni lililozinduliwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Makundi Maalum Dkt ,Dorothy Ngwajima Kulia ,kushoto Kwa Mkuu wa Wilaya Diwani wa Kipunguni Steven Mushi na Mwenyekiti wa Mtaa wa Amani Daniel Malagashimba