Na Mwandishi wetu,TimesMajira
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamad Hassan Chande,amewataka wahitimu wa Chuo Cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki Tabora (BTI) kutumia vyema ujuzi na maarifa waliyopata wakiwa chuoni kuanzisha miradi mbaliymbali ya ufugaji nyuki katika kujiongezea kipato na kujikwamua kiuchumi.
Chande maesema hayo Mkoani Tabora wakati wa Mahafali ya 30 ya Chuo hicho ambapo amesisistiza wahitimu hao kuanza kujiajiri na kujiingizia kipato kutokana na maarifa waliyonayo, fursa za rasilimali za misitu ya asili na fedha za ruzuku kutoka serikalini kwenda kwa wafugaji nyuki waliopo hapa nchini.
“Niendelee kusisitiza kwa wahitimu wetu kutumia ujuzi mlioupata hapa Chuoni kwenda kuanzisha miradi midogo midogo ya kufuga nyuki ili kujipatia kipato. Serikali kupitia Wizara mbalimbali na taasisi zake itaendelea kuwatengenezea mazingira wezeshi ili muweze kufanikiwa katika miradi mtakayoanzisha” amesisitiza Chande.

Aidha, amewasihi wanafunzi kuheshimu walichinacho kwa kutumia maarifa hayo katika kujipatia maendeleo ikiwa ni pamoja na kuzingatia nidhamu, uzalendo, uvumilivu, subra, ari ya kufanya kazi huku akisisitiza kuongeza jitihada kwenye ubunifu, kutotumia mitandao ya kijamii kinyume na taratibu na sheria za nchi ili kujinufaisha.
Chande amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuongeza fursa za ajira kwa vijana kwenye sekta ya ufugaji nyuki kwa kuendelea kuajiri wakufunzi wapya kwenye chuo hicho hatua itakayosaidia kuondokana na uhaba wa wakufunzi na maendeleo ya sekta hiyo yenye umuhimu mkubwa katika ukuaji wa uchumi na pato la taifa.

Katika hatua nyingine Chande ameelekeza uongozi wa chuo hicho kuendelea kukitangaza chuo hicho ili kufahamika na watanzania wengi wafahamu uwepo wa chuo hicho, kuendelea kusimamia fedha na miradi inayotekelezwa katika chuo hicho, kuimarisha mashirikiano na wadau na vyuo vingine kwa ajili ya kuongeza ufanisi, ubunifu na tafiti.
Jumla ya wahitimu 181 wamehitimu mafunzo hayo kwa ngazi ya Stashahada na Astashahada ya ufugaji Nyuki.



More Stories
Rhino Rangers yapewa nguvu ya kupanda Ligi Kuu
Barrick North Mara yazindua Wiki ya Mahusiano.
AFDB kuipatia Tanzania Dola Milioni 26 za Mabadiliko ya Tabianchi