Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Waziri wa Madini Dk.Doto Biteko amesema kuwa Wizara ya Madini imejipanga kukusanya jumla ya Shilingi za Kiatanzania Bilioni 894.3 kwa mwaka wa fedha 2022/23 sawa na ongezeko la asilimia 22.12 ikilinganishwa na Bilioni 696.4 zilizopangwa kwa Mwaka wa Fedha 2021/22.
Dk Biteko amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari akiwa wilayani Bukombe mkoani Geita wakati akifafanua utekelezaji wa vipaumbele vya bajeti ya wizara kwa mwaka wa fedha 2022/23.
Ameeleza kuwa kati ya fedha zitakazokusanywa, Bilioni 822.0 sawa na asilimia 91.9 zitakusanywa na kuwasilishwa hazina na Bilioni 72.3, sawa na asilimia 3.1 zitakusanywa na kutumika na taasisi zilizo chini ya Wizara.
Amesema kuwa mwaka wa fedha 2021/22 wizara ilikusanya Bilioni 622.5 sawa na asilimia 96 ya lengo iliyopangiwa (bilioni 696.4), mchango wa wachimbaji mdogo ukiongezeka hadi asilimia 44 mwaka 2021/2022 ukilinganisha na asilimia 30 ya mwaka wa fedha 2020/2021.
More Stories
SACP Katabazi Elimu ya usafirishaji wa kemikali muhimu kwa watanzania
REA yajitosa kwenye nishati safi ya kupikia
Maghorofa Kariakoo mikononi mwa Tume