Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online
WAZIRI wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dkt. Doto Biteko ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendelea kuboresha maslahi ya watumishi na kuweka mazingira wezeshi mahala pa kazi ikiwemo kwa wauguzi.
Aidha, Bukombe tunatambua mchango mkubwa unaotolewa na wauguzi katika kuimarisha Afya zetu, tunatakiwa kuwalinda na kuendelea kuwapa ushirikiano uliyobora kwa Sababu hao nao ni binadamu ili kuhakikisha wanafanya kazi yao kwa weledi.
Ameyasema hayo Mei 17, 2023 Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dkt. Doto Biteko wakati akiongea na Watumishi wa Idara ya Afya wa Wilaya ya Bukombe katika Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi duniani ambapo kitaifa iliadhimishwa Mei 12, jijini Mwanza.
Waziri Biteko amewatia moyo wauguzi wote kwa kutambua kazi kubwa wanayoifanya Bukombe baada ya kusikiliza changamoto zao na kuahidi kuendelea kuzifanyia kazi ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha maslai kwa watumishi wa Sekta ya Afya.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba amempongeza Waziri Dkt. Biteko kwa jinsi anavyoungana na sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya na kuwaomba wauguzi kuendelea kumuunga mkono Mbunge ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Dkt. Deograsia Mkapa amesema wauguzi wa Bukombe nao wameungana na Wauguzi wote duniani katika kutambua mchango wao kwa jamii ni asilimia 80 ya huduma zote katika Sekta ya Afya na kutoa shukrani za Sekta ya Afya kwa Waziri Dkt. Biteko kufadhili jambo hilo.
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini