January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Biteko amtaka Katibu Mkuu mpya Wizara ya Madini kuifanya Wizara hiyo kuwa kivutio kwa watanzania

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.

Dkt.Biteko amesema hayo jijini hapa leo,Machi 10,2023 wakati akizungumza katika  kikao maalumu cha Wizara na Taasisi zilizochini ya Wizara ya madini na kumtambulisha Katibu huyo  kwa watumishi wa idara zote za Wizara hiyo kikiwa na lengo ni kumpitisha katika katika mambo mbalimbali ili ajue wapi kwa kuanzia katika majukumu yake.

WAZIRI wa Madini,Dkt.Doto Biteko amemtaka Katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo,Kheri Mahimbali aifanye Wizara hiyo kuwa kivutio cha kila mtanzania kutamani kuja  kufanyakazi Wizara hiyo.

Amesema kuwa kutokana na muda mwingi watumishi kuutumia wakiwa kazini katibu mkuu anatakiwa kuwafanya waajiriwa hao kujiona wao ni wa muhimu katika wizara hiyo.

“Mfanye ambaye hataki kufanya kazi yake aifanye mbinu gani utatumia unazijua vizuri mimi sitaki kukufundisha lakini pia  mfanye kila mtanzania atamani kufanya kazi wizara ya madini karibu sana wizara ya madini nakutakia kilaraheli”amesema Dkt.Biteko.

 Dtk.Biteko ameendelea kumsisitiza Katibu Mkuu huyo kuwa katika wizara hiyo wapo watu wa aina mbalimbali ambao katibu mkuu atakwenda kufanya nao kazi hivyo anapaswa kuwa makini ili kuhakikisha kazi zinafanyika na kufikia malengo ya serikali.

“Ndugu katibu mkuu hapa unaowaona wapo watu wa kila aina wapo ambao ukiwapa kazi wao wanaangalia dead line hata kama kazi uliwapa haijakamilika wanakuletea, lakini wapo ambao kazi hawamazili kwa wakati hawakabidhi kwasababu hazijakamilika,

wapo ambao wao kazi hawafanyi kabisa, lakini wapo wengine ambao wao ukiwapa kazi wanafanya na ukiwarekebisha wanafurahi lakini wengine hawataki  kurekebishwa ukiwarekebisha wanakukasirikia”amesema Dkt. Biteko

Hata hivyo Dkt.Biteko amemkabidhi majukumu ya kuyafanyia kazi katibu mkuu mpya wa wizara hiyo ikiwemo kuwafanya waajiriwa wa Wizara hiyo kujiona wao ni wa muhimu kutokana na muda mwingi watumishi hao kutumia wakiwa kazini ili kusimamia malengo yaliyowekwa na serikali yakamilike.

Kwa upande wake Naibu waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa, amesema yapo mambo mengi ambayo wameyafanyia kazi hadi sasa ikiwemo kupunguza idadi ya watu waliokuwa wamekaimu katika nafasi mbalimbali.

“Katibu mkuu nashukuru kuwa umeeleza kuwa unapaenda kufanya kazi kama timu mie pia ni muumini wa ushirikiswaji lakini toka nimeingia madarakani katika nafasi hii mambo mengi tumeyafanyia kazi ikiwemo kupunguza idadi ya watu waliokua wakikaimu katika nafasi mbalimbali.

“Hivyo tunakuomba katika nafasi ambazo bado hazijafanyiwa kazi uone ni namna gani zinafanyiwa kazi ili maeneo yanayokaimiwa yapate watu na kazi ziendelee kwa malengo tuliyojiwekea”amesema Dkt. Kiruswa

Naye Naibu katibu Mkuu wa Wizara hiyo Msafiri Mbibo ameesisitiza ushirikiano na umoja,uvumilivu upendano na utendaji kazi kwa kiwango cha umahili wa juu kwani  mambo hayo hayawezi kujitokeza yenyewe bali ni kutokana na uongozi bora.

“Nichukue fursa hii kumuhakikishia katibu mkuu mpya kwamba anakuja katika taasisi au sekta inayoongozwa na viongozi wapenda watu,Wapenda Mungu na wenye weledi na wanaongoza watu wenye sifa hizo hivyo nataka kuhakikishia umekuja kwenye timu bora kwahiyo  natumia fursa hii kukukaribisha sana katika wizara yetu.

“Madini ni sekta kubwa katika taifa linaloendelea na liliondelea sasa kwavile Tanzania tumepewa jukumu hili sisi  basi tutaendelea kuiendeleza sekta hii na nisisitize mambo matatu Weledi,uadilifu na Uwajibikaji.