Na Mwandishi Wetu,TimesMajira,Online, Chato
NAIBU Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amezidua Kiwanda cha Pamba cha Chato (CCU) na kuielezea hatua kama mpango kabambe wa serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli wa kujenga
sekta ya kilimo inayojitegemea sambamba na uhakika wa upatikanaji wa malighafi.
Akizungumza mara baada ya kukizinduzi wa Kiwanda cha Pamba cha Chato (CCU) mwishoni mwa wiki, Waziri Bashe alisema kufufuliwa kwa kiwanda hicho ni mwanzo mzuri kwa wakulima wa pamba kuongoza uzalishaji na kuinua vipato vyao.
“Mradi wa kufufua kiwanda hiki umegharimu jumla ya sh. 6,714,804,447 kutoka katika benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) lengo likiwa kuimarisha sekta ya kilimo ili kuwanufaisha wakulima wa pamba,” amesema Bashe.
Amesema kufufuliwa kwa kiwanda hicho ambacho kilisimama kufanya
uzalishaji kwa miaka kadhaa kutawafanya wakulima wilayani Chato na
maeneo mengine ya jirani kuongeza uzalishaji na hivyo kuleta unafuu wa maisha kwa wakulima.
“Serikali imedhamiria kuifanya sekta ya kilimo inajitegemea kwa kuwa mbali ya kutoa ajira kwa Watanzania walio wengi, lakini pia imekuwa na mchango wa asilimia 25 katika pato la Taifa,” amesema.
Aidha, waziri Bashe amepongeza Benki ya Kilimo kwa jitihada zake za kuwaletea wakulima maendeleo kwa kuwapa mikopo yenye mashrti nafuu jambo ambalo linaongeza tija katika ukuaji wa uchumi wa Nchi.
“Natoa pongezi kwa TADB, Wizara, wadau wa kilimo pamoja na chama cha ushirika wilayani chato (CCU) kwa namna tulivyoshirikiana kuhakikisha kiwanda hiki kinaendelea na uzalishaji na hivyo kuchochea uzalishaji wa zao la pamba,” amesema na kuziomba taasisi zingine za fedha kujitokeza na kuwekeza katika sekta ya kilimo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Japhet Justine amesema kuzinduliwa kwa kiwanda hicho kutaongeza thamani ya zao la pamba ambayo ilishuka tangu msimu wa 2013/14.
“Tunaamini hatua tunazochukua kwa mazao ya kimkakati ikiwemo zao la pamba iyasaidia katika kuongeza thamani yake na hivyo kuwa na bei ambayo itamfanya mkulima anufaike zaidi na kuchungia ukuaji wa pato la Taifa,” amesema.
Alisema bei ya msimu huu imekuwa nzuri ukilinganisha na misimu kadhaa ya hapo awali na kwamba wataendelea kuimarisha upatikanaji wa soko zuri na lenye faida kwa mkulima.
“Msimu unaomalizika tulijitahidi kununua pamba kwa wakulima kwa bei ambayo waliifurahia lakini tunaendelea kuweka mikakati ya kulifanya zao la pamba kuwa na faida zaidi kwa kufufua viwanda vya kuchakata pamba kama hiki cha Chato,’’ amesema Bashe.
More Stories
Bodaboda wamchangia Rais Samia Mil 1 ya fomu ya Urais
CCM hakuna kulala, Nchimbi atua Tabora kwa ziara ya siku mbili
Kongamano la Uwekezaji na Biashara lafunguliwa Pwani