January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wazindua kitabu cha uongozi uliotukuka wa JPM

Na Dotto Mwaibale,TimesMajira Online

MUUNGANO wa Maaskofu zaidi ya 15 na Wachungaji 100 mwanzoni mwa wiki wamezindua kitabu kinachoelezea uongozi uliotukuka wa Rais Dkt. John Magufuli.

Kitabu hicho kimeandikwa na Mtendakazi katika Shamba la Bwana, Restoration Bible Church Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi wa kitabu hicho kiitwacho Uongozi Uliotukuka, JPM ni Kiongozi wa Kisiasa na Kiroho, uliofanyika jijini Dar es Salaam, uliongozwa na Askofu Mkuu wa Makanisa ya Naioth Gospel Assemblies of God, ambaye pia ni Katibu Mkuu mstaafu wa Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste Tanzania, Dkt. David Mwasota.

Dkt. Mwasota amesema, lengo la kuandikwa kitabu hicho ni kutazama uongozi wa Rais Magufuli kwa pande za kisiasa na kiroho.

Askofu huyo amesema katika utendaji kazi wake, Magufuli anamtegemea Mungu hivyo kumfanya aonekane anaiongoza nchi kwa upande wa kiroho.