April 19, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wazee wawili jela maisha kwa kubaka na kulawiti

Na Esther Macha, Timesmajira Online Mbeya

MAHAKAMA ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya imewahukumu kifungo cha Maisha jela  wakazi wawili wa wilaya hiyo kwa makosa  ya kubaka na kulawiti watoto wadogo wa kike.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Chunya James Mhanuzi  machi 5,2025 na Mwendesha mashitaka wa Serikali wakili Mwajabu Tengeneza  .

Mshitakuwa wa kwanza Antony Mwangoka (53) mkazi wa Mbugani Chunya alimbaka na kumlawiti mtoto mwenye (9).

Mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo Disemba 17,2024 katika Kijiji cha Mbugani Wilayani Chunya mkoani Mbeya.
 
Amesema kuwa mshitakuwa huyo alikamatwa Disemba 22, 2024 na kufikishwa mahakamani na kutiwa hatiani kwa makosa mawili ya kubaka na kulawiti

Mama mzazi wa mhanga alibaini tukio hilo wakati akifua nguo za ndani za mtoto wake baada ya kukuta zimechafuka na alipomchunguza mtoto wake alibaini kubakwa na kulawitiwa na Anthony  Mwangaka.

Mkazi mwingine wa  kibaoni Chunya aitwaye Said kandonga (60)amehukumiwa kifungo cha Maisha gerezani kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka (8).

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Chunya
James Mhanuzi na Mwendesha mashitaka wa Serikali wakili Mwajabu Tengeneza Aprili Mosi, Mwaka huu

Mshitakiwa alitenda kosa hilo Septemba 16, 2024 katika Kijiji cha Kibaoni Wilayani Chunya na alikamatwa Oktoba 02, 2024 na kufikishwa mahakamani ambapo alitiwa hatiani kwa kosa la kubaka.

Siku ya tukio Mshitakiwa aligundua kuwa nyumbani kwa Mhanga mzazi wake hayupo ndipo aliingia ndani ya nyumba kisha kumbaka Mhanga na wakati anaendelea kutenda kosa hilo alikutwa na mama mzazi wa mtoto huyo ambaye alitoa taarifa Polisi ndipo ulifanyika msako na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa ambaye alihojiwa na kufikishwa mahakamani ambapo alitiwa hatiani.