BARAZA la Wazee wa Wilaya ya Kahama (UWAKA), wameiomba serikali kuitungia sheria sera yao itakayoelekeza katika utekelezaji wake kisheria.
Ombi hilo limetolewa juzi na Katibu UWAKA, Paul Ntelya ambapo alisema sheria hiyo itungwe ili ielekeze utekelezaji katika mambo ya msingi juu yao.
Ntelya amesema sera ya wazee ipo kwa miaka 17 toka mwaka 2003, lakini hadi sasa haina sheria yoyote inayoelekeza utekelezaji wake kisheria.
“Sera yetu ipo toka mwaka 2003 hadi sasa haina sheria yoyote, sasa imefika wakati naiomba serikali itunge sheria itakayoelekeza utekelezaji wake katika mambo ya msingi kwenye kuwahudumia wazee,” amesema Ntelya.
Ntelya amesema katika moja ya sehemu ya sera hiyo, inasema wazee watalipwa pensheni lakini hadi sasa utekelezaji wake, umekuwa haupo kwa sababu ya kutokuwepo kwa sheria yoyote inayoelekeza hivyo.
More Stories
Rais Samia apeleka Bil. 6 kuboresha sekta ya elimu Kaliua
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo