Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbarali
Wazazi na walezi jijini Mbeya,wameshauriwa kujenga tabia ya kukaa na watoto wao na kuwahimiza umuhimu wa kujisomea vitabu mbalimbali ambavyo vitawapa uwezo wa kujifunza zaidi na kuwajenga kielimu.
Kauli hiyo imetolewa na Mwandishi wa vitabu na Muandaaji wa mashindano ya Kusoma vitabu kwa watoto kutoka Jamhuri ya Zech,Chris Lameck,ambaye amesema usomaji huo wa vitabu utasaidia kujenga jamii itakayokuwa bora kwa miaka ya badaaye.

“Nashauri jamii kujenga utamaduni wa kujisomea ili kujenga uelewa na kuongeza maarifa,nawaasa wazazi na walezi kuwa karibu na watoto kujenga utamaduni wa kujenga uelewa,”amesema Lameck.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa shirika la Mama na Mtoto,Edgar Mlawa, amesema”Tumepata vitendea kazi na namna ya kufundisha wanawake kupitia watoto wao, hii ni njia mojawapo kwetu hata serikali inaweza kutusaidia ili kuokoa kizazi cha sasa na kuweka malengo,”amesema Mlawa.
Veronica Ndeshiga ni Katibu wa shirika la Mama na Mtoto, amesema kuwa lengo la kuandaa mashindano hayo ya kusoma vitabu ni kufanya tathimini ya watoto.
Veronica amesema,kupitia mashindani hayo wamebaini changamoto ya baadhi ya watoto kuacha kusoma vitabu lakini kupitia mashindano hayo wanaamini wataendelea kujisomea vitabu ili waweze kujijenga zaidi.
Frank Kachulu ni mwanafunzi wa shule ya msingi Mahango,amesema faida ya kujisomea vitabu inasaida watoto kupata elimu ilio bora ambayo itakuwa msaada katika kujijenga kimasomo na uelewa.

Katika mashindani hayo watoto walipata fursa ya kucheza michezo mbalimbali ikiwemo kuvuta kamba, kukimbia na yai kwenye kijiko pamoja na kusoma ambapo washindi walipatiwa zawadi ikiwemo madaftari,begi na kalamu.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako