Na Esther Macha,TimesmajiraOline,Chunya
WAZAZI na walezi wilayani Chunya mkoani Mbeya wametakiwa kutenga muda wa kuzungumza na watoto wao ili kuweza kufahamu changamoto ambazo zinaweza kuwa zinawakabili na kuzipatia ufumbuzi ikiwa ni pamoja kuwajenga kimaadili badala ya kuwaachia majukumu ya malezi walimu pekee.
Kauli hiyo imetolewa leo,Novemba 24,2023 na Mchimbaji wa madini ya dhahabu wilayani hapa Ambakisye Mwanjemba ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahali ya Nne (4)shule ya mchepuo wa kiingireza ya Holy Land Pre& primary School iliyopo katika Mji mdogo wa Makongolosi Wilayani Chunya.
Mwanjemba amesema kuwa wazazi wakiwapeleka watoto shule za bweni wanapunguza majukumu ya kuwalea watoto huku asilimia 100 wakiwaachia walimu kuwa walezi wa watoto na wazazi watafanya nini ipo haja kwa kila mzazi kuhakikisha kuwa anakuwa karibu na mtoto katika malezi.
“Ndugu wazazi tujipe majukumu walau ya asilimia 50 mtoto akiwa shule na akirudi nyumbani asilimia 50 ni wajibu wa mzazi lakini pia yawezekana kuna shida ngumu mtoto anapitia akiwa nyumbani na mzazi hajui na tulio wengi tupo bize na utafutaji wa maisha kama naliongea tofauti mtanambia , hata waliokuja hapa wengi wao ni wanawake akina baba hawapo kwasababu wapo bize na shughuli za maisha ndugu zangu wazazi tutenge muda walau wa kuwasikiliza watoto na kuwapokea walimu kuwalea watoto kwa sehemu msiwaachie walimu majukumu moja kwa moja “amesema Mwanjemba.
Aidha Mchimbaji huyo amesema kuwa ndiyo maana wakati fulani watoto walio wengi wanapenda kuwa shule kwasababu wakirudi nyumbani muda mwingi anakuwa na Dada wa kazi nyumbani kipindi cha likizo na kwamba wakirudi shule wanapata faraja kwa walimu zaidi yote sababu wazazi wanakuwa wamesahau majukumu yao hivyo ni vema kupunguza ubize kwa ajili ya watoto wao .
Akizungumzia kuhusu soko la ajira Mwanjemba amesema ifike wakati wazazi kusomesha watoto kwa gharama kubwa ikiwezekana ili kuwatengenezea matarajio ya ajira badaaye hata kama wanaenda kujiari lakini wanakuwa wameandaliwa vizuri , ni vema kusomesha watoto kwa gharama kubwa kwani ajira zimekuwa chache wakifika sehemu na kuwa elimu ya kutosha wataenda kushindanishwa na waajiri hivyo ni vema kupambana sababu soko la ajira limepungua.
’Mwajiri anapoangalia anajua huyu anafaa na hili wazazi tusitegee kabisa katika kuwapa elimu bora kwa watoto , lakini pia nipongeze shule hii ya holyland kwa kulea watoto katika maadili ya kidini mnafanya jambo kubwa sana , malezi ya kidini ni muongozo wa mtoto anapokwenda niwaombe ndugu zangu mtafute shule nzuri zenye maadili ya dini ili muweze kuwapeleka watoto wenu,”amesema Mwanjemba .
Akizungumza na Timesmajira Mkurugenzi wa shule wa Holy Land Pre &Primary school, Lawena Nsonda (maarufu kwa jina la Baba Mzazi)amesema kuwa mahafali hayo ya awali kwa shule hiyo ni ya Nne na kusema zaidi ya wanafunzi wa awali 31 wamehitimu.
Nsonda amesema kuwa kwa kushirikiana na walimu na wazazi wameweka mnyonyoro mmoja katika kufanya kazi kwa usawa kwa kuhakikisha watoto wamekula vizuri , wamelala vizuri nqa kupata elimu bora iliyo na malezi mazuri.
Akizungumzia kuhusu mazingira ya usalama wa watoto amesema mabweni ya watoto wa kiume na kike yapo mbali mbali na kila bweni lina mwalimu ambaye analinda usalama wa watoto na kuwatunza pamoja na kuwa na masomo ya kuwafundisha watoto na hata kipindi cha likizo wanafundisha watoto kutokubali kupakatwa na mtu yeyote pia shule hiyo ina mwalimu wa saikolojia ambaye kazi yake kubwa ni kuangalia watoto ambao hawako sawa ambao huwa jirani na mwalimu huyo na kueleza changamoto zao.
Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo Mwalimu Yona Mwakalinga amesema kuwa shule hiyo ilianza mwaka 2019 ikiwa na wanafunzi wawili(2) na mwalimu mmoja na jingo moja lenye vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja (1) na kwamba ilipofika mwaka 2020 shule hiyo ilipata usajili kamili kwa namba EM.18174 ikiwa ni shule ya awali ya kutwa ambapo ilikuwa na wanafunzi 65 na kuwa mpaka sasa shule hiyo ina wanafunzi 420 kati yao wasichana ni 219 na wavulana ni 201.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa