November 15, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wazazi watakiwa kufatilia maendeleo ya watoto wao

Na Heri Shabaaban,timesmajira,Online

MKURUGENZI wa Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo,Neema Mchau amewataka wazazi kusingatia Elimu katika kufatilia Maendeleo ya watoto wao wasome mpaka kufikia vyuo Vikuu ili Serikali iweze kupata viongozi bora.

Mchau ameyasema hayo katika mahafali ya 17 Shule ya Msingi Ulongoni ambapo alikuwa mgeni rasmi katika shule hiyo ambapo amewaasa Wazazi kuzingatia elimu kwa kuwaendeleza watoto waweze kusoma kumaliza darasa la saba sio mwisho wa Elimu kwani elimu aina mwisho watoto wana haki ya kupata elimu bora.

“Taifa lolote ili liweze kuendelea Wananchi wake lazima wapatiwe elimu bora sio bora elimu nawaomba wazazi na jamii kwa ujumla marufuku tusiwapeleke watoto kwa ndugu baada kumaliza elimu ya Msingi kwani bado watoto wana haki ya kuendelea na elimu ya sekondari mpaka vyuo kumaliza elimu ya Msingi sio mwisho wa Elimu” amesema Mchau

Amesema Dunia imeharibika katika kipindi cha utandawazi kila mzazi ana jukumu la kulea mtoto wake mwenyewe kwa Usalama wa Watoto wetu sio busara kumpamtu mtoto wako akulelehe .” wazazi mnatakiwa kuzingatia elimu na kuunga mkono juhudi za Serikali za elimu bila malipo katika kuwasimamia watoto waweze kusoma na kuwa viongozi wa baade,”amesema

Aidha amesema katika sekta ya elimu inawaibua wataalam wengi wakiwemo wataalam,Madaktari,Mawaziri ,Waandisi,Wabunge ,Mawaziri kutokana na msingi bora wa elimu ambao jamii watawekea vizazi vyao.