December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

wazazi walindeni watoto dhidi ya mmomonyoko wa maadili

Judith Ferdinand,TimesMajira Online Mwanza

Wito umetolewa kwa wazazi na jamii kuwafuatilia watoto wao ili kuwalinda na vitendo viovu hususani vilivyoibuka hivi karibuni vya ushoga vinavyosumbua dunia.

Wito huo umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt.Angeline Mabula,wakati wa ziara yake ya kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kipindi cha miaka miwili ya Rais Samia Suluhu Hassan,ambapo alitembelea na kukagua shule mpya ya msingi ya Kahama na Shibula, maabara katika zahanati ya Kahama, ujenzi wa ofisi ya serikali ya mtaa wa Kabambo Kata ya Kiseke pamoja na shule ya Angeline Mabula.

Dkt.Angeline ameeleza kuwa kuna hatari ambayo imeingia sasa kwa sababu ya mitandoa na kuiga vitu visivyo faa,masuala ya ushoga ninyi mnajua,watoto wetu wanaharibika,sisi hatujaumbwa hivyo wazazi mkemee na mfuatilie watoto wenu.

Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt.Angeline Mabula,akusikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wa shule ya sekondari Angeline Mabula iliopo Kata ya Kiseke,wakati alipotembelea shule hiyo.

Ambapo ameeleza kuwa maadili yamemomonyoka kwa sababu wazazi wameacha wajibu wao wa kule na kuruhusu watoto walelewe na watu wengine kila mzazi atimize wajibu wake kwenye malezi na afanye yeye ili wale wengine wawe msaada tu.

Ameeleza kuwa ikiwa Mungu alipomuumba mwanadamu angempa Mussa na Abdalah peke yake wasingezaliana vivyo hivyo kwa mwanamke angemuumba Asha na Maria wasingeijaza dunia.

“Hili la ushoga linaenda kupoteza maadili ya mtazania kwasababu mwanaume na mwanaume au mwanamke na mwanamke hawawezi kufanya kitu chochote,warudi kuanzia kwenye maadili ya kidini suala la ushoga liko kinyume na dini, mila na desturi za mwafrika,”ameeleza Dkt.Angeline na kuongeza kuwa

Pia akitumia msemo wa Hayati Magufuli kuwa binadamu tusizidiwe akili na wanyama, kama wazazi wasiwaonee haya watoto wao lazima wawafuatilie na ikiwezekana wawaogeshe hata kama watoto wana miaka nane waogeshe iwapo watakuwa wameanza vitendo hivyo mzazi utajua tu.Huku akiwataka wazazi kutoa taarifa pale wanapobaini mtoto wa kiume anatembea ndivyo sivyo.

Sanjari na hayo akiwa shule ya sekondari Angeline Mabula, Mbunge huyo amechangia kiasi cha milioni 1.95 kwa shule hiyo kwa ajili ya kuwanunulia wanafunzi wenye uhitaji sare huku nyingine ikiongezea katika upungufu wa fedha uliopo kwa ajili ya kukamilisha maabara.

Kati ya fedha hizo kiasi cha 950,000 kwa ajili ya kuwanunulia sare za shule wanafunzi 100 kati ya 215 ambao wenye mahitaji maalumu huku milioni 1, kwa ajili ya kuongeza fedha zilizopungua katika ujenzi wa maabara wa shule hiyo.

Dkt.Angeline amechangia kiasi hicho wakati akizungumza na wazazi pamoja na wanafunzi katika mkutano uliofanyika shuleni hapo mara baada ya kusikiliza kero za wananchi pamoja na changamoto za shule hiyo ikiwa ni moja ya ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo jimboni humo.

Ambapo ameeleza kuwa Rais Samia katika Wilaya ya Ilemela upande wa elimu sekondari ameisha tuletea kiasi cha zaidi ya bilioni 5.52,ambazo zimejenga madarasa,kuweka madawati na kila kitu kinachopaswa kuwekwa.

Mbali na hayo Dkt.Angeline amewataka wazazi kuhakikisha wanatoa mchango wa chakula shuleni ili kuwasaidia wanafunzi waweze kupata mlo wakati wakiendelea na masomo.

“Mwanafunzi anapopata chakula shuleni anakuwa na akili ya utulivu na inamfanya asiwe na njaa na asiweze kuwaza mambo mengine isipokuwa elimu tu,”.

Akizungumzia ujenzi wa shule hizo mpya za msingi Dkt.Angeline ameeleza kuwa serikali imeamua kujenga shule mpya katika jimbo hilo ili kuwasaidia wanafunzi wanaotembea umbali mrefu waweze kusoma mazingira ya karibu lakini pia kumpunguzia na changamoto alizokuwa anakutana nazo njiani wakati wakienda shule.

Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt.Angeline Mabula akishiriki ujenzi wa choo cha shule mpya ya msingi Shibula Kata ya Shibula alipotembelea shule hiyo.

Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa vyumba vya madarasa,ofisi ya walimu na matundu ya vyoo shule ya msingi mpya iliopo Kata ya Kahama Mtendaji wa Kata hiyo Victor Leonard, ameeleza kuwa ujenzi huo umegharimi kiasi cha milioni 100.95.

Lengo ikiwa ni kupunguza umbali mrefu wa wanafunzi kutembea pamoja na kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani kwa shule ya msingi Kahama.

Muonekano wa baadhi ya madarasa ya shule mpya ya msingi Kahama

Mkuu wa shule ya sekondari Angeline Mabula,Majaliwa Gerena, ameeleza kuwa changamoto iliopo katika shule hiyo ni upungufu wa fedha kiasi cha milioni 13 kwa ajili ya ukamilishaji wa maabara ambapo shule ilipokea milioni 30 ambayo haikudhi mahitaji ya ukamilishaji huo.