January 7, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wazazi saidieni serikali kuibua vipaji vya watoto wenye ulemavu

Na Esther Macha,Timesmajira,Online, Mbeya

WAZAZI na walezi wameombwa kuisaidia serikali kuibua vipaji vya watoto wenye ulemavu walivyopewa na Mungu ili waweze kulitumikia Taifa lao na kulitendea haki kundi hilo.

Imeelezwa kuwa wapo watoto  wenye ulemavu ambao wamesimamiwa vizuri  na wazazi  mpaka sasa ni viongozi wa nchi  ,changamoto waliyo nayo haiwafanyi kutokuwa na uwezo wa   kushindwa kujifunza  na kuleta tija katika nchi yao.

Ofisa Elimu kata ya Mapogoro Wilaya ya Mbarali  ,Francis Makombe alidema wakati akizungumza na Times majira ofisini kwake juu ya mikakati ya kuwaibua watoto wenye ulemavu katika kata hiyo .

Makombe amesema kuwa kuna watoto wengi wenye ulemavu  lakini wazazi na walezi wanashindwa kuwatendea haki kwa kudhani kuwa hawawezi kufanya chochote  hivyo kukata tama na baadhi kushindwa hata kuwapeleka shule.

“Niwasihi wazazi na walezi kusaidia serikali kuibua vipaji vya watoto wenye ulemavu ili kuweza kuitendea haki  nchi kwani wapo watoto wengi wenywe ulemavu wenye uwezo  wa kuwa na vipaji mbali mbali  lakini vinashindwa kuonekana kutokana kukosa sapoti kutoka wazazi “amesema Mratibu huyo.

Akielezea  jitihada za wadau Makombe amesema kwamba kuna wadau ambao wamekuwa wakijitokeza kusaidia watoto waliopo katika katika mazingira magumu wakiwemo watoto wenye ulemavu waliopo katika kata ya Mapogoro wilayani hapa.

Hata ameeleza kuwa  asasi zisizokuwa za kiserikali zimekuwa zikifanya jitihada  za kupita nyumba kwa nyumba kuibua watoto wenye ulemavu  katika kuisaidia serikali ili watoto waweze kupata haki ya kupata elimu

Mabadaga ipo shule ya Msingi na tuna watoto wenye ulemavu  wa aina tofauti ambao wapo tisa (9)kutokana na  wilaya hiyo kutokuwa na shule wanalazimika kuwachanganya na wanafunzi wengine katika shule ya msingi Katumba (2) iliyopo wilayani Rungwe mkoani mbeya ”amesema Makombe.

Eliza Lutanile ni mkazi wa Isenyela amesema jamii ya Mapogoro imekuwa na mwamko mzuri wa kuwatoa  watoto wenye ulemavu kwa jamii ili waweze kupata haki yao ya kimsingi ya kupata elimu .

“Tunashukuru haya mashirika ambayo yamekuwa yakitutembelea kutupa elimu ya malezi ya watoto wetu hawa wenye ulemavu kujua haki ,kufuatia na tumegundua tuna watoto wengi wenye vipaji mbali mbali “amesema. Lutanile mkazi wa Isenyela.

Mbunge wa Jimbo la Mbarali , Francis Mtega amesema kuwa zipo jitihada mbali mbali ambazo zimekuwa zikifanywa na maofisa maendeleo ya jamii wa kata na wilaya katika kuwatambua watoto wenye ulemavu.