Na Angela Mazula,TimesMajira Online
WAWEKEZAJI hapa nchini wamefurahia soko la bidhaa wanazozalisha na wameamua kujipanga kuongeza Uzalishaji zaidi ili kuendana na Tanzania ya viwanda na Uchumi wa Kati.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa kampuni ya Vehicle Assemblers (GFA) Imran Kamali, ambaye amefika Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na kufanya kikao na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Dk. Maduhu Kazi wakiwa na lengo la kujadili chanagmoto mbali mbali na fursa za uwekezaji hapa nchini.
Kampuni ya GFA inayomiliki kiwanda pekee cha kwanza nchini cha kuunganisha magari ambacho kwa sasa wameanza na uunganishaji wa Maroli (Trucks) ambayo yatampunguza gharama ya uagizaji magari hayo nje ya nchi hali itakayoweza kuimarisha na kupandisha bidhaa zetu kwa kutotumia fedha za kigeni katika kuagiza magari nje ya nchi.
Naye Mkurugenzi wa Kituo cha uwekezaji nchini Dk. Kazi amewakaribisha wawekezaji kuiona fursa hiyo na kuichangamkia kwa kuanzisha miradi mingine kwenye eneo hilo kupitia TIC ili kunufaika na vivutio vya kiuwekezaji ambavyo Serikali imeboresha zaidi kwa ajili ya miradi ya aina hiyo.
Mradi huo wa pekee umesajiliwa TIC mwezi Februari 2020 na unatarajia kuanza uzalishaji wake mwezi Septemba mwaka huu huko Kibaha. Huku Watanzania takribani 100 wamepata ajira kwenye awamu ya kwanza ya utekelezaji na kiasi cha dola za Kimarekani milioni 2.5 kimewekezwa ambacho ni sawa na fedha za Tanzania Shs 5.5 billion.
Hata hivyo Mkurugenzi wa GFA Imran Karmali amesema, anashukuru kwa ushirikiano alioupata na anaoendelea kuupata kutoka kwa viongozi mbali mbali wa Serikali katika Kuhakikisha wanafanikiwa katika kufanikisha kuanza kwa mradi huo.
Amesema, mpaka kukamilika kwa mradi huo kutaongeza soko la ajira kwa Watanzania katika Nyanja tofauti kuanzia katika ngazi ya mafundi na hata watoa huduma mbalimbali pia watahakikisha wanazalisha magari kwa soko la ndani na nje ya nchi hasa kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.
More Stories
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito