January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wawekezaji wa Dubai wahakikishiwa usalama na ZIC

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

MAONESHO ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Falme za Kiarabu (Dubai) ambapo Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) linawakaribisha Kuwekeza Visiwani Zanzibar kwa Uwekezaji na Kuwahakikishia usalama wa uwekezaji na Mali zao wakati wote wakiwepo Visiwani humo

Akizungumza katika Falme za Kiarabu (Dubai) Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la (ZIC) Arafat Haji amewakaribisha wadau Kuwekeza Visiwani Zanzibar na kupitia Shirika hilo linawahakikishia usalama wa uwekezaji wao kutokana na Shirika hilo kuwa na uzoefu na masuala ya bima za aina mbalimbali.

“Wawekezaji tunawapa Elimu ya namna gani wataweza kuwa na uwekezaji wenye usalama na kuhakikisha kunakua na Ajira ya Muda mrefu Ili kuleta tija na kukuza uchumi na maslahi ya Taifa.”

Aidha,Haji ameeleza kuwa wawekezaji wanapoamua kushirikisha (ZIC) wanafanya maamuzi sahihi kwani wapotayari kuwapa Miongozo ya kusimamia uwekezaji huo na kuhakikisha Mitaji yao inaleta Manufaa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima (ZIC) Arafat Haji akizungumza akiwa katika Maonesho ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Falme za Kiarabu (Dubai) na kuwataka wawekezaji watumie Shirika hilo kujihakikishia usalama