Na Bakari Lulela,Timesmajira
WAUMINI kutoka madhehebu ya kidini wajitokeza kwenye viwanja vya Leaders club jijini Dar es salaam kushiriki maombi maalumu ya kuliombea Taifa dhidi ya majanga mbalimbali.
Waumini hao walifika mapema Ili kusubili Dua hiyo maalumu kutoka kwa viongozi wa madhehebu mbalimbali ya kidini yaliyokuwa yameandaliwa kuendesha programu za maombezi kwa watanzania na waumini walifika kwenye viwanja hivyo.
“Maombezi ya wengi kama ilivyo katika viwanja hivi hupokelewa moja kwa moja na mungu kwa kusikia kilio maombi ya wengi na kusudio lao,” baadhi ya waumini wamesema
Aidha maombi hayo yaliwashirikisha viongozi kutoka madhehebu mbalimbali ya kidini akiwemo mtume Boniface Mwamposa na kuhani Mussa na wengineo katika Imani ya ukristo.
Hata hivyo maombi hayo yalikwenda sambamba na burudani za muziki wa injili kutoka kwa mwanadada Christina Shushu na wengineo.
Hata hivyo kwenye maombi hayo mgeni rasmi alikuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa ambaye alimuwakilisha Rais Dkt.Samia Suluhu Hassani
More Stories
Rose Mhando:Msama ni Baba kwangu acheni kunigombanisha naye
Watanzania watakiwa kudumisha amani
Dkt.Samia aipongeza Oryx,ataka wadau kupeleka gesi maeneo ya vijijini