Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline, Mbozi.
WATUMISHI wanne katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe wamekamatwa na Jeshi la Polisi wakituhumiwa kuharibu vielelezo vya ushahidi ili kumlinda Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Iporoto,Dkt.Nyamosi Rioba (34) ambaye alikamatwa Julai 19, 2023 kwa tuhuma za wizi wa dawa na vifaa tiba ili asiweze kupatikana na hatia.
Taarifa za uhakika toka ndani ya Hospitali hiyo na baadae kuthibitishwa na jeshi la polisi zinadai kuwa, watumishi hao wanatuhumiwa kuchezea vielezo ambavyo ni dawa na vifaa tiba vilvyokamtawa na kuhifadhiwa hospitalini hapo, vikimhusu Mganga Mfawadhi wa zahanati hiyo ambaye tayari amefikishwa mahakamani kwa makosa ya wizi wa dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi 1,066,120.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Theopista Mallya, alithibitishwa kukamatwa kwa watumishi hao na kwamba wataunganishwa katika kesi ya wizi wa dawa na vifaa tiba ambayo inamkabili Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Iporoto.
“Mtuhumiwa (Rioba ) alikamatwa na kuhojiwa kisha kufikishwa mahakamani Julai 31, 2023, wakati upelelezi zaidi ukiendelea kuhusiana na tukio hilo, ilibainika kuwapo watumishi wengine wanne walioshiriki katika wizi huo ” alifafanua Kamanda Mallya.
Aliwataja watumishi hao wanashikiliwa kuwa ni Muuguzi Mkuu Hispitali ya Wilaya ya Mbozi, Abdalbertha Haule, Mfamasia na mteknolojia dawa, Prosper Johnson, Mratibu wa kifua kikuu na ukoma, Stephano Kiluka, pamoja na Simoni Komba ambaye ni msimamizi wa huduma za maabara katika Hospitali hiyo ya Wilaya ya Mbozi.
Julai 19,2023, Jeshi la polisi Mkoa wa Songwe kwa ushirikianao na wananchi lilimkamata Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kijiji cha Iporoto, wilayani Mbozi, Dkt. Rioba kwa tuhuma za wizi wa dawa za binadamu mali ya serikali pamoja na vifaa tiba katika zahanati hiyo ya kijiji.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi