Na Moses Ng’wat, Timesmajira Online,Mbozi
Watumishi wa Mahakama mkoani Songwe,wameonywa kuepuka vitendo vya u vonevu,kwani haki na usawa ni msingi muhimu katika kujenga jamii yenye amani.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Farida Mgomi,kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo,wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Sheria nchini, uliofanyika Januari 25, 2025, ambapo kimkoa, imefanyika uwanja wa Stendi ya Malori, mjini Vwawa.
Mgomi ,amesema watumishi wa Mahakama wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na uwajibikaji wa hali ya juu, wakizingatia misingi ya usawa, utawala bora, na haki kwa wote.
Huku akiwahimiza wananchi kuepuka kuchukua sheria mkononi na badala yake kufuata taratibu za kisheria katika kutafuta suluhisho la migogoro yao.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Songwe, Radwell Mwampashi,amesisitiza umuhimu wa kuwafikia wananchi wa pembezoni ambao mara nyingi hawapati haki zao kutokana na kutokuwa na elimu juu ya mambo ya sheria.
Naye, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Songwe, Francis Kishenyi, amesema kuwa, wiki ya sheria ni fursa ya kipekee kwa Mahakama kuzungumza na wadau wake kuhusu changamoto na mafanikio katika mfumo wa sheria.
Kauli mbiu ya Wiki ya Sheria mwaka huu, “Tanzania ya 2050: Nafasi ya Taasisi Zinazosimamia Haki Madai katika Kufikia Malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo,”.
Katika maadhimisho hayo, taasisi za kisheria zitatoa huduma za bure za kisheria kwa wananchi kwa muda wa siku saba, ikiwa ni pamoja na ushauri wa kisheria na ufumbuzi wa matatizo.
More Stories
Serikali yazidi kuwakosha wawekezaji wadau waipa tano
Uwoya ampongeza Rais Samia kupitia Kampeni ya Jembe ni mama
Kishindo Mkutano wa Nishati leo, kesho Dar