Na Mwandishi Wetu, Timesmajiraionline, Zanzibar
WATUMISHI wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), wameshiriki Kongamano la tatu la ufuatialiaji na tathimini unaofanyika Zanzibar na kushirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali.
Mbali na watumishi hao, pia walengwa na wanufaika wa mfuko huo wameshiriki mkutano huo na kuonesha bidhaa mbalimbali wanazozalisha ambazo ni matunda yaliyotokana na TASAF.
Akizungumza leo mtaalam wa masuala ya TEHAMA wa Mfuko huo, Peter Lwanda, alisema lengo la kushirki katika mkutano huo ni kujifunza na kuongeza ujuzi kwenye suala zima la kufanya tathimini na ufuatiliaji.
“Kitengo kama hiki sisi TASAF tunacho muda mrefu, lakini kwa sababu tunafanya Ufuatiliaji na kufanya tathimini kwenye miradi yetu mbalimbali, mkutano huu ni muhimu kwetu kuongeza ujuzi na kuendelea kujifunza ili kuwa na uhakika wa kufanya kazi kwa ufasaha,” alisema Lwanda
.
Aidha, ameweka wazi TASAF wamekuwa wakiendesha miradi mbalimbali Zanzibar na katika mkutano huo pia kulikuwa na maonesho ya mafanikio yaliyofikiwa na walengwa wa mfuko huo visiwani Zanzibar.
“Lakini kwenye suala la tathimini, sisi pia tumekuwa tukijitathimini kwa kutumia wataalam kutoka nje ya TASAF tukiamini hatuwezi kujitathimin wenyewe kama tunataka matokeo sahihi, na kikubwa ni kuhakikisha malengo ya mfuko huu yafakiwa katika kila miradi yake,” alisema.
Mkutano huo wa tatu ulioanza Septemba 17 na kushirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali na ulimelizika leo .
More Stories
Waziri Mkuu: Tumieni matokeo ya tafiti za kisayansi katika utekelezaji wa mipango ya kitaifa
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu