March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watumishi Nkasi wapigwa msasa uandaaji wa mpango, bajeti

Na Israel Mwaisaka, Timesmajira Online+Nkasi

Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa,imeendesha mafunzo maalum kwa watumishi wake kuhusu uandaaji wa mipango na bajeti,yenye lengo la kuimarisha ufanisi,matumizi ya rasilimali pamoja na utekekalezaji wa vipaumbele.

Mafunzo hayo yamefanyika Oktoba 13,2025,yalilenga kuwajengea uwezo watumishi, wakuu wa idara na vitengo wa halmashauri hiyo,ili kuelewa mchakato wa kupanga bajeti kwa njia sahihi, mafunzo yaliyoendeshwa kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Nkasi.

Wawezeshaji wa mafunzo hayo ambao pia ni Maofisa Mipango Wilaya ya Nkasi, Ajaye Nguvila na Renatus Panda,wamesema dhumuni la mafunzo hayo ni kufundisha mbinu za kuandaa mipango ya shughuli (action plans) zinazoweza kutekelezeka ndani ya bajeti

Pia kutoa ufahamu juu ya mfumo wa kitaifa wa mipango na bajeti (kwa mfano system za PlanRep).

Kwa upande wa watumishi walioshiriki mafunzo hayo wamesema wamepata uelewa juu ya mchakato na uandaaji wa bajeti na mipango, hivyo kuongeza uwezo wao wa kuandaa bajeti bora kupitia idara na vitengo vyao.