Na Mwandishi wetu, Timesmajira
Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imefanya tafrija ya mwaka wa fedha 2025/26 huku ikitoa wito kwa watumishi kuongeza umoja, mshikamano na uwajibikaji mahala pa kazi.
Hafla hiyo imefanyika jana usiku katika jengo jipya ofisi ya Tume makao makuu lililopo Njedengwa mkoani Dodoma, lengo ni kutambua mchango wa watumishi wanaojitoa zaidi katika utendaji kazi pamoja na kuimarisha mahusiano miongoni mwa wafanyakazi wa taasisi hiyo.Tafrija hiyo imehudhriwa na watumishi wa NIRC kutoka nchi nzima.
Akizungumza katika tafrija hiyo iliyokutanisha watumishi zaidi ya 300 ambapo
178 kutoka mikoani na wengine 122 kutoka Makao Makuu na watoa huduma zaidi ya 30, Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Raymond Mndolwa amewapongeza watumishi kwa utendaji kazi, wenye lengo la kuleta matokeo katika sekta ya Kilimo.
Mapema kabla ya hafla hiyo watumishi hao walishiriki vikao vya Baraza la Wafanyakazi na semina za kitaaluma zilizofanyika siku mbili kabla

Amesema kuwa vikao hivyo vimekuwa nyenzo muhimu ya kukumbushana wajibu wa kisheria na kimaadili ambao watumishi hao wana wajibu kwa wananchi wa Tanzania kusimamia sekta ya Umwagiliaji nchini.
Mndolwa ametoa shukrani za dhati kwa Bodi ya Uongozi Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa usimamizi thabiti, pamoja na Menejimenti na Wahandisi wa Umwagiliaji wa Mikoa (RIE) na watumishi wote kwa ushirikiano wao uliotukuka.

Aidha Mndolwa amesisitiza kuwa mafanikio ya taasisi yanategemea uimara wa familia ya watumishi hao ambapo amewaasa kuendelea kufanya kazi kwa bidii na uaminifu ili kufikia malengo ya Serikali kuongeza eneo la Umwagiliaji.

More Stories
ACT Wazalendo yaingia mazungumzo ya kisiasa kwa maslahi ya Zanzibar na wananchi wake
Wanaume Summit 2026 kukutanisha washiriki zaidi ya 2,000
Chongolo, azindua kampeni ya “Linda Ushirika, Chagua Uadilifu”