April 1, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watuhumiwa 227 wakamatwa Februari 27 hadi Machi 27,2025

Na Judith Ferdinand na Daud Magesa,Timesmajira Online, Mwanza

JESHI la Polisi mkoani Mwanza limefanikiwa kukamata watu 227 katika oparesheni iliofanyika Februari 27 hadi Machi 27 mwaka huu kwa tuhuma mbalimbali za makosa ya kijinai na usalama barabarani.

Kati ya watuhumiwa hao kupatikana kwa noti bandia 7, kujihusisha na vitendo vya uhalifu 104, kupatikana na pombe haramu 56, zana haramu za uvuvi 6, matumizi ya dawa za Kulevya 14.

Ambapo watuhumiwa 125 wamehojiwa na kufikishwa mahakamani na kesi zipo katika hatua mbalimbali huku kati ya kesi hizo 73 zilipata mafanikio kwa watuhumiwa kupatikana na hatua na kufungwa vifungo mbalimbali gerezani.

Hayo yameelezwa Machi 28,2025 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP.Wilbroad Mutafungwa, amesema miongoni mwa kesi mbili za ukatili wa kijinsia kwa watoto zilizofikishwa mahakamani,washtakiwa wamehukumiwa miaka 30 jela kila mmoja.

Mutafungwa amesema, katika tukio moja Wilaya ya Ilemela, Athuman Morandi (36) , dereva wa pikipiki, alikamatwa kwa tuhuma za kumchoma kwa kitu chenye ncha kali na kumsababishia kifo  Mhochi Joseph (29) ,baada ya kumfumania akiwa amelala na mke wake ndani ya nyumba yake.

Katika tukio lingine wilayani Sengerema, Doto Marco (18) alikamatwa kwa tuhuma za kumchoma Eliyas ​​John (18)  na kitu chenye ncha kali kifuani na kumsababishia kifo ambapo chanzo cha tukio ni ugomvi uliozuka baina yao.

Wengine 125 walikamatwa kwa tuhuma za uhalifu wa aina mbalimbali, ikiwa ni pamoja na biashara ya dawa za kulevya, matumizi ya zana haramu za uvuvi, pombe haramu na kukamatwa wakiwa na noti bandia (Dola ) za Marekani.

Sanjari na hayo amesema katika ajali za barabarani, jeshi la Polisi Mwanza limefanikiwa kudhibiti kwa kiasi kikubwa,ambapo kwa kipindi cha mwezi mmoja jumla ya makosa 6,896 yalikamatwa na kutozwa faini.

Ambapo makosa hatarishi 1,540 yamekamatwa na baadhi ya madereva kufungiwa leseni zao.Makosa hayo ni kuendesha gari kwa mwendo kasi, dereva kuendesha gari akiwa amelewa pamoja na kuendesha gari bovu.

magari 34 yaling’olewa namba za usajili nankutakiwa kufanyiwa matengenezo huku bajaji 75 na pikipiki 92 zinazovunja sheria ya usalama barabarani zimekamatwa Katia kipindi hicho.

lilikagua magari na kuendelea na operesheni dhidi ya madereva wanaokiuka sheria ambapo makosa 6,896 yalibainika huku madereva 1,540 kukamatwa kwa makosa ya mfumo hatarishi.

DCP utafungwa alieleza baadhi ya madereva waliobainika kufanyia kazi mifumo hatarishi iliyofutiwa leseni kwa miezi sita, magari mabovu 34, bajaji 75, na pikipiki 92 zilikamatwa kwa kuvunja sheria za barabarani.