December 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watu zaidi ya 20 wajishindia zawadi Kampeni ya upige mwingi mpaka Afcon

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

WATU zaidi ya 20 wamejishindia zawadi mbalimbali kutoka Kampuni ya simu ya Airtel kupitia kampeni ya upige mwingi mpaka Afcon.

Baadhi ya zawadi zilozotolewa ni simu za mkononi, televisheni aina ya smart, pikipiki, jokofu na fursa ya kwenda kushuhudia Mchuano ya Mataifa ya Afrika(Afcon)

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 6, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati akiendesha droo ya nne ya kampeni hiyo, Meneja Mahusiano kutoka Airtel, Jennifer Mbuya, amesema kampeni hiyo ilianza mwezi januari mwaka huu na itaendelea kwa siku 90, na ndani ya wiki hii kampuni hiyo itaambatana na baadhi ya washindi kwenda nao nchini Ivory Coast kushuhudia michuano ya Afcon.

“Tunatoa rai kwa Watanzania kutumia huduma za Airtel wajishindie zawadi hizi na kupata fursa ya kwenda kushuhudia michuano ya Afcon,”alisema.

Kwaupande wake Mkazi wa Magomeni Dar es Salaam, Sophia Mnywaki mmoja wa washindi ambaye amejishindia simu ya mkononi, alishukuru kampuni hiyo ya simu kwa zawadi, huku akitoa rai kwa Watanzania kutumia huduma zaidi wajishindie safari ya kwenda nchini Ivory Coast.

Naye mshindi mwingine aliyejinyakulia zawadi ya simu ya mkononi, Ali Zungu alisema mashindano hayo ni ya kweli na ameipata kupitia kutumia mara kwa mara huduma za kampuni hiyo.

Meneja Mahusiano wa Airtel Tanzania Jennifer Mbuya (kulia) na Meneja Huduma wa Airtel Tanzania, Irene Ngomuo (kushoto) wakimzawadia simu ya Tecno Spark 20 mkazi wa Dar es Salaam, Sofia Mnyuwaki