Na mwandishi wetu, TimesMajira Online
Jeshi la Polisi nchini limetoa taarifa ya mauaji ya watu watatu wakiwepo askari wawili wa Jeshi la Uhamiaji na mwananchi mmoja yaliyotokea katika kijiji cha Mtakuja, Kata ya Lulembela, Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita.
Misime amewataja walio uawa katika tuki hilo ni Mkaguzi wa Jeshi la Uhamiaji Salum Msongela Mpole na Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Gilbert Edward, ambao wote kituo chao cha kazi ni wilaya ya Bukombe.
Samabamba na hilo amemtaja Mwananchi aliyeuawa katika tukio hilo kuwa ni Juma Bundala mkazi wa Kijiji cha Mtakuja. Pia amesema kuwa askari mmoja konstebo wa uhamiaji amejeruhiwa katika tukio hilo ambapo alikimbizwa hosptali kwa matibabu zaidi.
SACP Misime amesema kuwa chanzo cha tukio hilo la mauaji ni baada ya askari hao kufika katika kijiji hicho baada ya kupata taarifa za uwepo wa wahamiaji haramu katika nyumba ya mwananchi mmoja kijijini hapo amabapo amebainisha kuwa hadi sasa watu sita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kutokana na tukio hilo.
Amebainisha kuwa tayari Timu ya uchunguzi imeshatumwa kwenda katika kijiji hicho, kufanya uchunguzi wa mazingira yote yanayozunguka tukio hilo ili hatua ziweze kuchukuliwa kulingana na ushahidi utakaokusanywa na timu hiyo.
Aidha Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wa kijiji cha Mtakuja kuwa watulivu na kufuata sheria wakati wa uchunguzi ukiendelea.
More Stories
Jay-Z aunganishwa na P Diddy kwa kumdhalilisha binti wa miaka 13
Rais Samia afanya uteuzi
Waliombaka, kulawiti binti wa Yombo, Dar jela maisha