Na Stephen Noel,Mpwapwa
Watu 225041 wanatalajiwa kujiandikisha na kuboresha taarifa zao Katika daftari la wapiga kura Katika wilaya ya Mpwapwa yenye majimbo mawili ya uchaguzi Jimbo la Mpwapwa mjini na Jimbo la kibakwe Akifungua kikao kazi kaimu mkurugenzi mtendaji Halmashauri hiyo bwana Bahati Magumula amewasihi makundi mbalimbali Katika Jamii ya kuunganisha nguvu Katika uhamasishaji wa jamii juu ya kujitokeza katika kujiandikisha Katika daftari la kupiga kura.
Magumula amesema mala kadhaa wafuasi wa vyama vya siasa wamekuwa wakitoa malalamiko mwishoni mwa zoezi hivyo amewataka kuanza uhamasishaji wa wanachama wao kujitokeza kujiandikisha ili wakawe na sifa za kupiga kura.
Kikao kazi hicho cha Siku Moja kilicho wajumuisha wadau wa masuala ya uchaguzi kilichofanyika Katika ukumbi wa halmashauri ya Mpwapwa kiliwajumuisha Viongozi wa dini,wanasiasa,bodaboda,mama lishe, na makundi mbalimbali Katika Jamii.
Kwa upande wake Afisa uchaguzi Halmashauri ya Mpwapwa Thomas Magali amesema Katika zoezi Hilo linalotarajiwa kuanza Siku ya tarehe 11 octoba Hadi 20 octoba 2024 wanatarajia kuandikisha watu wapatao laki mbili elfu ishirini na Tano na arobaini na mmoja(225041).
Mmoja wa washiriki wa warsha hiyo mwenye UWAKILISHI wa watu wenye ulemavu, Filimon Masumega amesema lazima tume izingatie mahitaji ya watu wenye ulemavu ikiwa karatasi za maandishi nundu na maeneo rafiki vitakapo pangwa vituo vya kupigia kura.
Uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 utakuwa ni uchuguzi wa awamu ya saba tangu kuanzishwa Kwa uchaguzi wa VYAMA vingi hapa Nchini na zoezi Hilo linatarakowa kufanyika 27.Novomber 2024.
More Stories
Wizara ya madini yakusanya bil.521 nusu ya kwanza mwaka wa fedha 2024/25
Meya awafunda wenyeviti Serikali za Mitaa
Mgeja aipongeza CCM kwa uteuzi Wagombea Urais