Na Moses Ng”wat,Timesmajiraonline,Songwe.
KATIBU Tawala (RAS) wa Mkoa wa Songwe, Happness Seneda, ameshangazwa na idadi kubwa ya watoto walio na umri wa kuwa shule katika Wilaya ya Songwe kuonekana kwenye maeneo mbalimbali yanayohusisha shughuli za kiuchumi kama uchimbaji dhahabu na kilimo cha tumbaku.
Nakuziagiza kamati za usalama za kata na vijiji kuhakikisha watoto hao wanaondolewa kwani maeneo hayo sio salama kwao.
Seneda ameeleza hayo, Disemba 12, 2023 wakati akizungumza na watumishi wa umma wa Tarafa ya Songwe Wilayani Songwe, akiwa ameambatana na sekretarieti ya Mkoa ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku tatu kufuatilia miradi ya maendeleo katika Wilaya hiyo.
“Huku kwenu kuna changamoto ya watoto wadogo kuhusika kwenye shughuli za kiuchumi, ukipita kwenye maeneo ya mito unakuta watu wanachimba huku watoto wadogo nao na vikarai, hao wanaanza kuona fedha wakiwa wadogo sasa msipoweza kuwantro mapema ndio mambo yanayoleta shida,
“Lakini kuna kilimo cha tumbaku huko Gua na Ngwala nako watoto wanafanya shughuli hizo za tumbaku hivyo tujitahidi kuwafuatilia wataishia huko na hatutaweza kutengeneza kizazi mahususi cha kukimbizwa maendeleo nchi yetu ” amesisitiza Seneda.
Amesema Wilaya ya Songwe kupitia kamati za usalama katika ngazi za vijiji na kata wanatakiwa kuweka mkakati maalumu wa kuzuia watoto walio na umri wa kuwa shule hawapotelei kwenye shughuli za uchimbaji dhahabu.
“Jambo hilo mnatakiwa kuliwekea mkakati maalum kama Wilaya ili watoto wote wanaanza nalumaliza shule na hata wanapokuwa shuleni tuhakikishe umekuwa wa kiwango cha juu ya asilimia 90,”amesema Seneda.
Katika hatua nyingine, Seneda amewataka walimu kuwa karibu na wanafunzi ili kubaini vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa huku akisema kuwa mkoa huo utawashughulikia watu wanaochezesha au kuficha ushahidi wa naotuhumiwa kubaka au kuwalawiti watoto.
Ameeleza kuwa kumekuwa na wimbi la ubakaji na ulawiti watoto hivyo mkoa huo umeweka mikakati ya kuhakikisha ukatili huo unakomeshwa.
More Stories
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best
Waziri Mavunde:Benki Kuu yanunua tani 2.6 za Dhahabu nchini