Na David John TimesMajira Oniline, Dar Es Salaam
KAMANDA wa Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Willbroad Mutafungwa amesema uwepo wa Mahakama ya watoto ya ukiukwaji wa makosa ya Barabarani unasaidia kwa kiwango kikubwa kupunga ajali zisizokuwa za lazima.
Mutafungwa amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akishuhudia uendeshwaji wa mahakama hiyo na kusomewa mashtaka pamoja na kupewa hukumu kwa baadhi ya madereva waliokuwa wakifanya makosa na kufikishwa kwenye chumba maalumu katika shule ya msingi Olimpio iliyopo Upanga wilayani Ilala.
Amesema kuwa Mahakama hiyo inaleta msaada mkubwa katika jamiii na hasa katika kuondosha au kupunguza uwepo wa Makosa ya barabarani kwa madereva ambao wanashindwa kufuata sheria za barabarani zilizowekwa na mamlaka husika.
“leo nimekuja kushudia hapa mimi Mwenyewe uendeshwaji wa Mahakama hii ya watoto kwakweli watoto hawa wanauwezo mkubwa sana embu fikiria wanakuuliza maswali mtu mzima na unatoa ahadi na kiyapo cha kutorudia makosa jambo hili ni zuri na sis kama Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani tutaendelea kutoa ushirikishirikiano mkubwa kwa shirika hili la Amendi.”amesema Kamanda Mutafungwa.
Pia Kamanda Mutafungwa alilipongeza shirika la Amendi kwa kujitoa kwao na kazi kubwa wanayoifanya ya kuhakikisha wanatumia Mahakama hiyo ya watoto kutoa elimu.kwa madereva nchini nzima hususani kwenye maene ya mashuleni.
Niwapongeze sana Amendi wanafanya kazi kubwa sana katika kuhakikisha wanatoa elimu hii kupitia watoto hawa na sisi tutaendelea kutoa kila ya aina ya ushirikiano kwao.nakuyataka Mashirika mengine kujitokeza ili kuhakikisha ajali za barabarani zinamalizika”amesema .
Akizungumzia kuhusu Ajali za barabrani amesema kuwa kwa asilimia kuwa ajali zimepungua sana na wataendelea kutoa elimu ya usalama barabarani ili kuona mwisho wa siku ajali zinamalizwa kwa asilimia kubwa kama si kutokomezwa kabisa.
Kwaupande wake mkurugenzi mtendaji wa shirika la Amendi Simon Kalolo amesema kuwa wao kama wadau wa usalama barabarani kwakushirikiana na Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani kazi kubwa wanayofanya nikutoa elimu ya usalama barabarani.
Amesema kuwa katika kuhakikisha wanapunguza ajali hizo za usalama wa barabarani hivi sasa wamekuja na Mahakama ya watoto mashuleni ambayo kazi yake kubwa itakuwa ni kuwahukumu madereva ambao wanavunja sheria za alama za usalama barabarani na kusababisha ajali zisizo za lazima.
Amefafanua kuwa wamekuja na Mahakama hiyo ikiwa ni sehemu ya ubunifu kwa lengo la kufikisha meseji ya moja kwa moja kwa watumiaji wa vyombo vya moto kwani anaamini watumiaji wengi wanapohojiwa na watoto wadogo kwa makosa ambayo wanayafanya watajisikia vibaya na ni rahisi kubadilika.
” Huu ni ubunifu tu ambao sisi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani tumeufanya na kwakweli Mahakama hiii imekuwa ikifanya vizuri sana na hadi sasa tumeshazifkkia shule karibu nane na lengo nikuona tunatekeleza mradi huu kwa nchi nzima.”amesema Kalolo
Ameongeza kuwa watoto hao wamekuwa wabunifu na kwakweli wengi wao ukiwauliza wanasema wanatamani waje kuwa Mahakimu na hiyo ina tokana na uhodari na ujasili wanaouonyesha katika kuuliza maswali kwa madereva ambao wanafanya makosa hayo.
Nao watoto hao kwa pamoja wamesema madereva wanatakiwa wawe makini na wasiwachukulie poa kwa sababu wao ni watoto wadogo kwani wakifanya makosa na kufikishwa mbele ya Mahakama yao wajuwe watakabiliana na maswali magumu na watapata hukumu na kula kiapo cha ahadi cha kutofanya tena makosa ambayo yanapelekea kusababisha ajali hususani kwa watembea kwa miguu (vivuko)
More Stories
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari