January 14, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watoto milioni 50 kupatiwa chanjo

NEW YORK, Mkakati wa kimataifa wa chanjo unaoongozwa na Umoja wa Mataifa umezinduliwa kwa lengo la kuwafikia watoto zaidi ya milioni 50.

Watoto ambao wamekosa chanjo za kuokoa maisha dhidi ya magonjwa kama vile surua, homa ya manjano na ugonjwa wa homa ya mapafu, kwa sehemu kubwa ikiwa ni kwa sababu ya athari za janga la corona (COVID-19).

“Hata kabla ya janga hilo, kulikuwa na dalili za kutia wasiwasi kwamba tulikuwa tunaanza kupoteza msingi katika vita dhidi ya magonjwa ya watoto yanayoweza kuzuilika na watoto milioni 20 tayari wamekosa chanjo muhimu,”alisema Henrietta Fore, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF).

Kwa mujibu wa UNICEF, usumbufu uliosababishwa na janga la COVID-19 mwanzoni mwa 2020 ulimaanisha kuwa utoaji wa chanjo ulishuka kutoka chanjo bilioni 2.29 mwaka 2019, hadi dozi za chanjo zaidi kidogo ya bilioni mbili mwaka jana.