Na Israel Mwaisaka, Timesmajira Online,Nkasi
TAASISI ya watu Makini Technology ya mjini Sumbawanga mkoani Rukwa kwa kushirikiana na wadau wengine wametoa msaada kwa wanafunzi 61 wenye mahitaji maalumu,kama sehemu ya matendo ya huruma wanapouanza mwaka mpya wa 2025.
Akizungumza wakati wa kukabidhi misaada hiyo kwa watoto hao katika shule tatu za mjini Namanyere wilayani Nkasi,Mkurugenzi wa Watu Makini Technology Obeid Theofil Kasiano,amesema kuwa taasisi yake kwa kushirikiana na timu ya vijana wajasiriamali wamechangishana kiasi cha zaidi ya milioni 1.3,kuwanunulia mahitaji muhimu ya shule kama madaftari,rula,kalamu na penseli.
Amesema kuwa wao kama sehemu ya jamii wanaguswa na changamoto mbalimbali ambazo watu wengine wanakumbana nazo, ndiyo maana waliona ni vyema kuwashika mkono watoto wenye mahitaji maalumu, kwa kuchangishana kidogo kile ambacho Mungu ameweza kuwajalia.
Kasiano, amefafanua kuwa kwao jambo hilo imekuwa ni utaratibu wao ambapo kwa mwaka juu ni mara ya sita na kwa wilaya Nkasi ni mara ya nne na kuwa wataendelea kufanya hivyo huku wakifanya ushawishi kwa watu wengine kuendelea kujitoa kama wao katika kuwasaidia watu wenye uhitaji.
Shule zilizonufaika na msaada huo ni shule ya msingi Majengo,Isunta na Nkomolo ambapo Walimu wakuu wa shule hizo wamekua msaada katika kuwaainisha watoto hao ambao wamekua wanufaika wa misaada hiyo.
More Stories
Tanzania,Uingereza kushirikiana katika kuendeleza madini Mkakati
Kamati ya Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini yagawa vifaa vya ujenzi
Hatma mrithi wa Kinana kupatikana