Na Judith Ferdinand,TimesMajira Online Mwanza
Imeelezwa kuwa watoto na vijana wenye usonji wanakabiliwa na uhitaji wa bima za afya,elimu na vifaa wezeshi,hivyo jamii,wadau na serikali wameombwa kusaidia kutatua changamoto hizo.
Ili watoto na vijana wenye kundi hilo kuweza kupata huduma za afya kwa urahisi na kupunguza mzigo kwa wazazi na familia kwa ujumla.
Ambapo taasisi ya kusaidia watoto na vijana wenye usonji ya Living Together Autistic Foundation (Li-TAFO), kwa mwaka 2022,imefanikiwa kuwasaidia watoto na vijana wenye usonji bima za afya 150.
Akisoma risala Agnes Simkanga katika hafla ya chakula cha jioni ya kujumuika na watoto na vijana wenye usonji pamoja na uzinduzi wa kitabu cha safari ya ushindi ya mama na mtoto mwenye usonji kwa lugha ya kingereza,iliondaliwa na taasisi iliofanyika jijini Mwanza.
Ameeleza kuwa uhitaji wa huduma hizo kwa watoto wenye usonji ni mkubwa lakini kutokana na uwezo mdogo wa taasisi hiyo wameshindwa kuwafikia idadi kubwa ya watoto na vijana hao.
“Licha ya uwepo wa changamoto hizo, tunaendelea kufanya utekelezaji wa afya zetu kwa kujitolea na kushirikisha wadau na wahisani ili kuchangia kwa manufaa ya wa na vijana wenye usonji hivyo tunaomba viongozi,wadau na jamii mtuunge mkono katika hili,” ameeleza Agnes.
Mkurugenzi Mtendaji wa Li-TAFO Mhandisi Shangwe Mgaya, ameeleza kuwa mpango wa taasisi hiyo kwa mwaka huu wa 2022 ilikuwa ni kutoa bima za afya 300 lakini kwa sababu ya uwezo mdogo wanashukuru wadau mbalimbali ambao wamekuwa wakiguswa na wamewachangia ambapo wameweza kutoa bima za afya 150.
Mbali na watoto wenye usonji pia wanawasaidia watoto wenye changamoto nyingine ambapo wameweza kutoa baiskeli kwa watoto 10.
Ameeleza kuwa,wazazi wengi wanapokuwa wamezaa mtoto mwenye changamoto wanakuwa hawana nguvu ya kufuatilia cheti cha kuzaliwa cha mtoto hivyo taasisi yake imesaidia upatikanaji wa vyeti hivyo Kwa watoto wenye usonji ambao walikuwa hawana vyeti hivyo.
Pia ameeleza kuwa , wataendelea kuwa na makongamano mbalimbali kwani jamii inawachukulia tofauti watu wenye usonji kwani changamoto iliopo pia bado jamii na wazazi bado hawajauelewa vizuri usonji.
“Jamii inachukulia kuwa mtoto mwenye usonji ni laana na kama umemtoa mtoto kafara,jamii itambue kuwa watoto hawa wana haki kama walivyo wengine ikiwemo kusoma,kufurahia maisha kama mtu mwingine,”ameeleza Mhandis Shangwe.
Sanjari na hayo ameeleza kuwa,watoto wengi wenye usonji wanalelewa na mama kwa sababu mtoto anapopata changamoto mtu wa kwanza kulaumiwa ni mwanamke hivyo wawapende watoto hao wawatunze na wasiwanyanyapae.
“Wazazi wengi ni wanawake ambao wengi wao wametelekezwa na wanawalea wenyewe watoto wao wenye usonji kwa maumivu makubwa,kwa sababu mtoto anapopata changamoto mtu wa kwanza kukulaumu ni mme wako japo wapo wanaume wamekimbiwa na wake zao lakini wanawake ambao wamekimbiwa na wanaume ni wengi,”ameeleza Mhandisi Shangwe.
Aidha ameeleza kuwa changamoto ya usonji ni kubwa na wakati anaanza alidhani nchi nzima ni yeye pekee mwenye mtoto ambaye ana usonji baada ya kuanza kutangazwa na kutoa elimu watu wengi wanaongelea changamoto hiyo.
“Watu wengi sasa wanaongelea kuhusu watoto wenye usonji hivyo tunaomba viongozi na serikali kulichukulua suala la usonji kwa umaskini zaidi vinginevyo tutakuwa tunatengeneza bomu, kumlea mtoto mwenye usonji ni gharama,hivyo suala la usonji linazidi kuongezeka tunahitaji wataalamu na kituo ambacho kitawasaidia watoto hao kwani kujifunza kwao ni tofauti na watoto wengine,”ameeleza Mhandisi Shangwe.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Massala,aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa katika hafla hiyo, ameeleza kuwa serikali ya Mkoa na Wilaya waliahidi kushirikiana na taasisi hiyo na haita acha kwani imebeba jukumu zito la kuwaunganisha katika changamoto hii ya usonji.
Ambapo jamii imepata uelewa juu ya usonji ni nini,tatizo la usonji siyo la mtu mmoja linaweza kumpata mtu yoyote na hakuna aliyeomba kuzaa mtoto mwenye usonji.
More Stories
Balozi Nchimbi kuongoza waombolezaji mazishi ya Kibiti leo
Dkt.Tulia,apewa tano kuwezesha wananchi
Nkasi yajipanga kukusanya mapatoÂ