May 20, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watiwa mbaroni kwa kukutwa na silaha bila kibali Dodoma

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma

JESHI la polisi Mkoa wa Dodoma  linawashikiria watuhumiwa nne kwa kosa la kupatikana na silaha bila kuwa na kibali katika wilaya ya Dodoma mjini na Wilaya  Mpwapwa.

Akizungumza na waaandishi wa habari jijini hapa leo Mei 20,2025 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma SACP George Kabazi amesema kuwa Mei 17 mwaka huu majira ya saa kumi kamili jioni katika mtaa wa kikuyu mission jijini Dodoma walikamatwa watuhumiwa wawili wote wakazi wa kikuyu mission wakiwa na bastola ikiwa na risasi 13 kwenye magazine yake.

Pia amesema Mei 19 mwaka huu majira ya saa kumi  na moja kamili jioni katika mtaa wa Lukole wilaya ya Mpwapwa walilamatwa watuhumiwa wegine wawili wakiwa na silaha iliyotengenezwa kienyeji inayotumia risasi za Shortgun iliyokatwa mtutu na kitako pamoja na risasi tano.

“Vilevile Mei 18 mwaka huu majira ya saa nne na Dakika 40 usiku katika mtaa wa Mbuyuni kata ya kizota jijini walikamatwa Nestory Kimario (38)na Thomas Paschal maarufu kwa jina la Sigan(28)wote wakazi wa Mbabala.

“Watuhumiwa hawa wamekutwa na mafuta aina ya Dizeli lita 2420 yakiwa kwenye madumu 89 yaliyoifadhiwa kwenye gari aina ya toyota yenye namba za usajili T273BKB,”amesema

Hata hivyo Kamanda SACP Katabazi amesema katika msako wamekamata vifaa mbalimbali vya kuvunjia Tv sita,Radio saba,ambazo zinadaiwa kuwa mali za wizi.

Hivyo ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa huo kwa kutoa taarifa za watu ambao wanadhani kuwa wanaweza kuwa na viashiria vya uhalifu ili waweze kutiwa nguvuni.