Na Heri Shaban, TimesMajira Online, Ilala
Mkuu wa Mkoa wa Dar ea Salaam Amos Makala ,amewataka WATENDAJI wa Serikali wa Mkoa huo wakiamka asubuhi wawaze kukamilisha Ujenzi wa madarasa kwa wakati Ili Watoto waweze kwenda shule .
Mkuu wa Mkoa Amos Makala, amesema hayo Wilayani Ilala Kata ya Kivule wakati wa kuangalia ujenzi wa madarasa 40 Kata ya Kivule Sekondari ya misitu madarasa 15 na Sekondari ya Kerezange madarasa 25.
“Ninaagiza Watendaji wa Serikali wakilala wakiamka wawaweze kukamilika ujenzi wa madarasa Ili Watoto waweze kusoma wa darasa la awali,Elimu ya Msingi na elimu ya Sekondari ” alisema Makala.
Mkuu wa Mkoa Makala alisema dhumuni la ziara yake endelevu kuangalia kampeni ya kujenga madarasa ya fedha za Serikali Shilingi bikioni 12 zilizotolewa na RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Alisema Mkoa Dar es Salaam wanafunzi zaidi ya Elfu 88 Rais ametoa fedha hizo amepunguza kero ya Madarasa kila mwaka .
Alipongeza Wilaya ya ILALA kwenda na wakati wamefikia hatua nzuri ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ya kuanza Wanafunzi Kidato cha kwanza .
Katika hatua nyingine amepongeza fedha za SERIKALI kuwafikia Walimu moja kwa moja na kusimamia miradi ni uwajibikaji mzuri Serikali inaendelea kuwaamini Walimu wa Ilala .
Alisema katika fedha za Serikali Shilingi bilioni 12 Wilaya ya ILALA wamezielekeza bilioni 6.4 ambazo fedha nyingi zimeelekezwa Jimbo la Ukonga kwa mbunge Jerry Silaa kwa ajili Jimbo hilo Lina eneo kubwa .
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija alisema mahitaji ya Madarasa Ilala madarasa 610 Mpaka January kutakuwa na madarasa 621 Wanafunzi wote wataenda Kidato cha kwanza .
Mkuu wa Wilaya Ludigija amewapongeza Kata ya Kivule na Liwiti viongozi wa CCM kuwa karibu na miradi ya Serikali kwa ajili ya utekekezaji wa Ilani ya Chama .
Mbunge wa Jimbo la Ukonga Jerry Silaa alisema Jimbo la Ukonga wamepokea jumla ya Shilingi bilioni 4 .6 kwa ajili ya kuziekeza sekta ya elimu kujenga madarasa kati ya fedha hizo Sekondari ya Misitu milioni 300 Kelezange milioni 340 zote pochi la Mama limefunguka .
Mbunge Jerry Silaa alimpongeza Mkuu wa Wilaya ya ILALA Ng’wilabuzu Ludigija,Meya wa Halmashauri ya Jiji Omary Kumbilamoto, Afisa Elimu Sekondari na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji kwa kufanya kazi kwa weledi na usimamizi mzuri miradi ya Serikali.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best