Na Zena Mohamed, Timesmajira Online,Mpwapwa
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Daniel Chongolo amewataka watendaji wa vijiji kuacha tabia ya kuuza maeneo yaliyotengwa na kuhifadhiwa kwajili ya matumizi maalumu kwani ndiyo chanzo za uharibifu wa mazingira.
Amesema Watendaji wa vijiji wanakawaida ya kuuza maeneo ambayo yamehifadhiwa kwa ajili ya matumizi maalum hivyo waache na badala yake wayalinde yasiharibiwe na mtu yoyote.
Chongolo amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Kingiti,Wilayani hapa ikiwa muendelezo wa ziara yake ya kutembelea majimbo yote ya Mkoa wa Dodoma ambapo amesema Mpwapwa kumekuwa na uharibifu mkubwa wa vyanzo vya maji 17 huku akitaka ufutiliaji katika vyanzo vyotr hivyo kama mboni ya jicho.
“Wewe ni mtendaji hapa mtu anaendaje kuharibu chanzo cha maji na wewe unaona,”alihoji Chongolo.
“Mimi nimewahi kuwa mkuu wa wilaya uliza kama kuna mtu aliweza kuibuka na kuharibu chanzo cha maji hao watendaji wote walikuwa wamenyooka, mtendaji ndio chanzo cha kwanza cha uhalibifu wa vyanzo vya maji,”amesema Chongolo.
Amesema kuwa watendaji wote kwenye maeneo yao wamepewa wajibu hivyo wanapaswa kutimiza wajibu wao wasikae kutengeneza urafiki wa kukusanya sadaka kwenye uhalibifu hilo halikubaliki kwasababu kesho na keshokutwa matatizo yanabebwa na serikali na wao ndio wawakilishi wa serikali.
“Hatuwezi kuwa na nchi ambayo kila mtu anaota sharubu na kufanya anachotaka lazima nchi iwe na utaratibu, lazima watu waheshimu sheria na waheshimu maeneo maalum yenye tija kwa nchi na si vinginevyo,”amesema Chongolo.
Aidha amesema kuwa mataraji ya CCM ni kumuona Mkuu wa Wilaya na kamati yake ya usalama ya wilaya ikianzisha mchakato wa operesheni kwenye vyanzo vya maji kwa kuweka alama, kuvilinda na kupanda miti kwani mtu yeyote anayeruhu uharibifu wa vyanzo vya maji ni mtu asiyetaka maisha ya kesho ya wananchi.
“Mtu akikuambia panda mpaka juu, hakutaki wewe, haitaki kesho yako, mimi ni kiongozi mwenye dhamana natamani sana muendelee kukipenda Chama cha Mapinduzi lakini mkipende kwa kuwambiwa ukweli na sio tofauti, mjue huo ndio msingi.”
“Mkuu wa Wilaya anawajibu wa moja kwa moja wa kusimamia hilo na si vinginevyo kama hawezi maana hatendi haki maana usimamizi wa kamati ya usalama ya wilaya ni wake na kama vyanzo vya maji vikiharibiwa ina maana hajatimiza wajibu wake.”amesema.
Chongolo amesema kuwa CCM inataka kuona vyanzo vya maji kote nchini vinawekewa alama na kulindwa na si vinginevyo na kuwataka wakuu wa wilaya kuhakikisha hilo linatekelezwa.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba