Na David John
ALIYEKUWA mkaguzi mkuu wa Serikali mstaafu Ludovic utouh amewataka watendaji wa Serikali kutekeleza mapendekezo yanayotolewa na CAG ili kuboresha usimamizi wa Rasilimali za Taifa.
Akizungumza katika uzinduzi wa kitabu cha ukaguzi wa uuma kiitwacho Misingi ya ukauguzi wa uuma (principle Public Sector Auditing) Ludovick uttouh amesema kuzinduliwa Kwa kitabu hicho kutawasaidia wananchi kuweza kuelewa namna ya Rasimali zao zilivyo tumika katika kuwaletea maendeleo.
Amesema Kuwa ripoti hiyo inaweza kutumika kama chanzo cha taarifa katika ufuatiliaji wa matumizi na Rasmali za uuma Kwa ngazi ya Halmashauri nakwamba ripoti hiyo inafafanua umuhimu wa ukaguzi namaoni ya ukaguzi pamoja na Mambo nane ambayo Serikali inatakiwa kuyafanyia kazi
Amesema Baadhi ya Mambo hayo ni pamoja na mwenendo wa Hati za ukaguzi,mwenendo wa utekelezaji wa mapendekezo ya CAG sambamba na maagizo ya kamati ya kudumu ya usimamizi ya Bunge ya Serikali za Mitaa.
“Ripoti hii imeandaliwa na taasisi ya wajibu Kwa ufadhili wa shirika la Maendeleo la ujerumani GIz nchini Tanzania kupitia Mradi wa usimamizi Bora wa Fedha za Umma (GFG).” amesema CAG mstaafu utouh .
Naye mgeni Rasmi katika uzinduzi huo Katibu mkuu kutoka wizara ya fedha Emmanuel Tutuba akizungumzia ripoti hiyo amesema Kuwa inakwenda Kuwa Msaada mkubwa Kwa serikali kwani inakwenda toa fursa kwa taasisi za umma kuona ni maeneo yapi yakwenda kufanyia kazi
Amesema taasisi hiyo ya wajibu chini ya mkurugenzi wake Ludovick Utouh anaipongeza mno kwa taarifa yao na wao Kama serikali wanakwenda kufanyia kazi maeneo yote ambayo yametajwa kama ni changamoto.
“kwakweli nawapongeza mno hii kazi ni kubwa na nawahakikishia kwamba taarifa hii tunakwenda kufanyia kazi na bahati nzuri taarifa imebainisha maeneo mbalimbali yanayopaswa kufanyia kazi” amesema katibu tutuba
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa