Na Penina Malundo ,Timesmajira
Washindi watatu bora waliibuka na zawadi mbalimbali msimu wa Tatu wa mnada wa Jukwaa la kidijitali la PIKU linalojihusisha na uendeshaji wa minada ya kipekee kupitia mtandao na kufanya jumla kufikia washindi tisa hadi sasa.
Wakitangazwa washindi hao na Meneja wa Habari na Mawasiliano wa PIKU Afrika, Barnabas Mbunda, alisema hii ni awamu ya tatu wa mnada huo unaoongozwa na Kampuni ya PIKU na kufanya kupata washindi mbalimbali.Akiwataja washindi hao ni pamoja na Jakson Ngonji, alijinyakulia Televisheni janja ya inchi 55 kutoka kampuni ya LG pamoja na ruta yenye kifurushi cha intaneti cha mwaka mzima, Jonathan Paul, alipata kombo ya bidhaa za kiume ikiwemo pafyumu, vidani vya mkononi, na saa ya kisasa na mshindi wa Tatu akiwa Niovita Shayo, alijishindia simu janja aina ya Samsung pamoja na spika ya Bluetooth. Mbunda, alisema kuwa ni mafanikio makubwa kuona zaidi ya washindi tisa wamejinyakulia zawadi mbalimbali kwa kushiriki mnada kwa njia ya kidijitali.Mambo yanazidi kunoga ambapo limeendelea kukabidhi zawadi kwa washindi wa awamu ya tatu ya promosheni yake.
” Piku Afrika ni Fahari kwani washindi katika minada yao wamepata bidhaa zao bila kikwazo, hali inayodhihirisha uwazi na ubunifu wa mfumo yao.

“Zawadi mbalimbali zilitolewa, ikiwa ni pamoja na “makombo” ya bidhaa kwa bei ya chini na ya kipekee.
Pia alisema kuwa bidhaa zote za kielektroniki ambazo washindi wamepata tayari zimekatiwa bima ya mwaka mzima, hivyo washiriki hawapaswi kuwa na wasiwasi kuhusu usalama au uimara wa bidhaa hizo,”amesema
Mbunda ameongeza kuwa promosheni inaendelea, na minada mikubwa zaidi bado iko mbele.
Ameeleza kuwa zawadi kuu kwa sasa ni gari aina ya Toyota Raum ikiwa ni zawadi ya funga mwaka.“Gari hiyo itatolewa pamoja na mafuta lita 100 kila mwezi kwa mwaka mzima, matengenezo ya bure kwa mwaka, bima kamili ya mwaka mzima.

Pia itatolewa pikipiki mpya aina ya TVS, itakayokabidhiwa ikiwa na helmeti na reflector, kadi ya mafuta lita 30 kwa kila mwezi kwa mwaka mzima,bima ya mwaka mzima,”amesema
Amesema tiketi za mnada kwa wale wanaotaka kushiriki, zinapatikana kwa Sh. 1,000 tiketi 10, sh. 5,000 tiketi 50, sh. 10,000 tiketi 100 na sh 100,000 tiketi 1,000.
Mbunda amesisitiza kuwa kadri idadi ya tiketi inavyoongezeka, ndivyo nafasi ya kushinda inavyokuwa kubwa zaidi.Kwa upande wake, Jakson Ngonji, mshindi wa kwanza wa Televisheni janja ya inchi 55, ameeleza kwa furaha namna alivyoshinda zawadi hiyo kubwa kwa kutumia dau dogo kupitia mfumo wa mnada wa kidijitali wa PIKU Afrika.
“Nilishiriki kwa matumaini na kwa kweli siamini hadi leo. Nawahamasisha vijana na Watanzania kwa ujumla wajitokeze kushiriki katika minada hii. Ni fursa ya kipekee kupata bidhaa za thamani kubwa kwa gharama ndogo,” amesema Ngonji.
PIKU Afrika inaendelea kuwa kinara katika mapinduzi ya minada ya mtandaoni, ikiwapa Watanzania fursa ya kupata bidhaa bora kwa bei nafuu kupitia mfumo wa kidijitali, wa uwazi, na wa kipekee.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako