Na Penina Malundo,Timesmajira
WATANZANIA wametakiwa kutunza miundombinu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kuacha tabia ya kuchoma Laini za Umeme na kuiba mafuta ndani ya Transfoma.
Aliyasema hayo leo jijini Dar es Salaam,Naibu Mkurugenzi Mtendaji Mipango,Utafiti na Uwekezaji kutoka TANESCO, CPA. Renata Ndege wakati wa semina ya wahariri na waandishi wa habari,amesema Shirika lao linaendelea kuweka mikakati mbalimbali ya kulinda miundombinu yao kwa kushirikiana na Serikali pamoja na wananchi.
Amesema kwa sasa TANESCO katika baadhi ya miundombinu yao wameweka mitambo ya Ulinzi ambayo inateknolojia ya hali ya juu katika ulinzi na endapo mtu akisogea inatambua.
“Tunatamani kuweka mitambo hii katika maeneo mengi lakini kutokana na gharama ya ununuaji wa miundombinu hiyo tunakwenda taratibu katika kuiweka kutokana na gharama hiyo ipo juu.
“Bado tunatumia ulinzi wa kutumia wananchi katika kusaidiana kulinda miundombinu yetu katika maeneo mbalimbali ili kuweza kusaidia miundombinu hiyo kuzidi kuwepo,”amesema.
CPA Ndege amesema kwa sasa TANESCO haina shida ya umeme kutokana na kuwepo kwa miradi mingi ya umeme ambayo inasaidia upatikanaji wa umeme kuwepo katika maeneo mbalimbali.
Amesema umeme unaokatika katika baadhi ya maeneo ni kutokana na ufanywaji wa maboresho na kuongeza uwezo wa yll utoaji wa umeme nchini ambao ni wa uhakika.
“Umeme upo ila tunachofanya ni kuboresha miundombinu yetu na kuongeza uwezo (Capacity)ambayo itasaidia kutoa umeme wa uhakika,”amesema.
Awali akijibu maswali ya waandishi wa habari na wahariri,Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu Wizara ya Nishati, Innocent Luoga amesema kutokana na uwepo wa miradi mingi nchini hali ya ukatikatikaji wa umeme unaenda kuisha baada ya miundombinu ya umeme kuimarisha.
Amesema bado kunakazi kubwa inaendelea ya kuboresha hali ya umeme kupatikana kwa wakati na mwaka huu baada ya kukamilisha baadhi ya ufungaji wa transfoma na hii ni kutokana na miradi kuwa mingi.
More Stories
Mwinyi: Kuna ongezeko la wawekezaji Zanzibar
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Maofisa Watendaji watakiwa kufanya kazi kwa weledi