Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Imeelezwa kuwa Moja ya njia kubwa inayotumika kushirkisha vyuo vya ndani na vyuo vya nje ni maonesho, hivyo Watanzania na Taasisi mbalimbali wametakiwa kuchangamkia fursa zinazopatikana katika Banda la Kampuni ya Global Education Link Ltd ili kujenga uhusiano, kujionea shughuli zinazopatikana katika handa hilo na kuongeza ushindani wa soko la ajira.
Wito huo umetolewa Jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Educational Link Ltd, Abdulmalik Mollel wakati akizungumza na wanahabari kwenye maonesho ya 47 ya Kimataifa ya biashara (Sabasaba).
“Moja ya njia kubwa inayofanyika Duniani huwa ni kupitia maonyesho, hapa sabasaba yapo makampuni mbalimbali kutoka nje ya nchi, yamekutana na makampuni mbalimbali kutoka ndani ya nchi hivyo maana yake uwezo wa kushirikiana katika upande wa trading ni mkubwa”
Mbali na hayo Mollel amesema juhudi mbalimbali zinaendelea kufanyika ili kuongeza idadi kubwa ya wanafunzi kutoka nje ya nchi kuja katika vyuo vya ndani hivyo vyuo vikuu nchini vimeshauriwa kuwekeza zaidi kwenye mafunzo ya vitendo ili imsaidie mhitimu kuwa na ushindani kwa vyuo vingine.
“Mafunzo kwa vitendo ni jambo la muhimu sana, hivyo mwanafunzi akiyapata mafunzo hayo yatamsaidia pale anapotoka chuo awe aliandaliwa kukidhi soko la ajira linalimzunguka”
Kadhalika Mollel,amewasihi watanzania wanaotaka kusoma katika vyuo vikuu mbalimbali nje ya nchi kuitumia taasisi hiyo ya Global Education link.
“Natoa wito kwa wanafunzi wote wanaotaka kwenda kusoma nje ya nchi waje kwetu tutawashauri na tutawaunganisha na Chuo husika”Amesema Mollel.
Kadhalika Mollel amesema itakapofika tarehe 17/7/2023 tume ya vyuo vikuu nchini itafanya maonyesho makubwa ya elimu ambayo yataisha tarehe 22/7 katika viwanja vya mnazi mmoja hivyo amewasihi wadau mbalimbali wa elimu kushiriki katika maonesho hayo.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi