January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watanzania 4494 wajishindia mamilioni ya pesa kampeni ya ‘Tigo cha Wote’

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

Ikiwa ni Takribani wiki mbili sasa tangu kampuni ya Mawasiliano ya Tigo izindue Kampeni yake ya CHA WOTE yenye lengo la kuwasaidia wateja wa Tigo kutimiza malengo yao waliojiwekea ndani ya mwaka huu , ambapo wateja zaidi ya 320 kila siku wanajishindia zawadi mbalimbali kama vifurushi vya Dakika na MB na kubwa zaidi Fedha Taslimu hadi Milioni tano kwa kufanya miamala tu kupitia TigoPesa.

Akizungumza Leo Julai 6, 2023. Wakati wa Kuwakabidhi Mfano wa Hundi Baadhi ya Washindi wa Milioni Moja Moja wiki ya Pili , Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa Bi. Mary Rutta amesema kuwa hadi sasa ikiwa ni wiki mbili tu tangu Kampeni iyo izinduliwe wameshapatikana washindi Takribani 4494 kutoka maeneo mbalimbali nchini .

” Leo tunayo furaha kubwa kuwa na baadhi ya washindi wa Wiki ya Pili wa Kampeni yetu ya CHA WOTE ambao hawa ni washindi wa Milioni Moja Moja kila mmoja, Lakini niwakumbushe Watanzania kwamba kila siku tunatoa zawadi ikiwemo pesa taslimu hadi Milioni Moja kwa washindi 320 ,kuibuka mshindi ni rahisi tu unachotakiwa ni kufanya miamala na Tigo Pesa kama Kutumia Lipa Kwa Simu , Kununua Vifurushi , Kulipia Bili kwa Tigo Pesa , n.k kwa kufanya ivyo nawewe siku si nyingi utakua miongoni mwa Washindi wa Kampeni hii ya CHA WOTE “. Alisema Bi. Mary Rutta.

Naye kwa Upande wake Josephine Mathew mfanyabiashara wa Mihogo ya kukaanga kutoka Mbezi Beach Dar Es Salaam amesema kuwa ana furaha kubwa kuibuka mshindi wa Kampeni hii na hakutegemea kama hata Watanzania wenye kipato cha kawaida wanaweza kushinda

” Kwakweli nikiri nimefurahi sana jamani , Mimi ni Nafanya biashara ya kuuza mihogo iliyokaangwa na huwa nafanya miamala mbalimbali kama kulipia bili , na kununua Vifurushi vya SMS na Muda wa Maongezi nafikiri ivyo ndo vimenifanya nkawa mshindi , kwakweli hakika hiii ni CHA WOTE maana kumbe inawezekana kila mtu akawa mshindi hata sisi wenye kipato cha kawaida ” Alisema Josephine Muda mchache baada ya Kukabidhiwa Hundi yake ya Milioni Moja Makao Makuu ya Tigo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.

Washindi wengine waliokabidhiwa Hundi ya Milioni Moja kila mmoja leo hii ni Zubeda Nicholaus Mfanyabiashara wa Keki – Mbezi Dar Es Salaam , Ridhiwan Rajabu Seleman Mkazi wa Morogoro na Grace Mathew Mallya Mkazi wa Mbezi Dar Es Salaam.