Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online. Tunduru
WAGONJWA watano sawa na asilimia 2.4 kati watu 203, waliobainika kuwa na ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) walioibuliwa kupitia kampeni ya uelimishaji na uibuaji ya ugonjwa huo inayofanywa na Hospitali ya Wilaya Tunduru mkoani Ruvuma, wamepoteza maisha katika kipindi cha robo ya tatu ya Julai hadi Septemba mwaka huu wilayani hapa.
Hayo yamesemwa mjini hapa na Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma wa Wilaya ya Tunduru, Dkt. Mkasange Kihongole katika kampeni ya uelimishaji na upimaji wa kifua kikuu kwa watu na makundi mbalimbali, wakiwemo mama lishe na waendesha bodaboda iliyofanyika kwenye Hospitali ya Wilaya Tunduru.
Amesema idadi hiyo ya vifo ni ongezeko la mtu mmoja, ikilinganishwa na watu wanne walipoteza maisha mwaka 2019 kati ya 145 waliokutwa na maradhi hayo kupitia kampeni hiyo.
Mratibu huyo amesema kwa upande wa watoto walio chini ya umri wa miaka 15 waliokutwa na kifua kikuu mwaka mwaka huu ni 75 sawa na asilimia 36.9 na mwaka 2019, waliokutwa na maambukizi ya kifua ni 25 sawa na silimia 17.2.
More Stories
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari