Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
SERIKALI kupitia bodi ya Utalii Nchini(TTB) inatarajia kupokea watalii takribani 1000 kutoka Taifa la Israel watakaoingia nchini kuanzia April tisa hadi 16 mwaka huu.
Hayo yamebainishwa Jijini Dar es Salaam leo na Mwenyekiti wa Bodi ya TTB Jaji Thomas Mihayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuongezeka kwa watalii hao ni matokeo ya Programu Maalumu ya Roya Tour iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kulitangaza taifa.
Jaji Mihayo amesema idadi ya watalii wa kimataifa imeongezeka kwa asilimia 48.6 kutoka watalii 620,867 mwaka 2020 hadi watalii 922,692 mwaka 2021
“Tumeendelea kupokea makundi ya watalii kutoka katika masoko yetu ya kimkakati yanayojumuisha Israel ambapo wiki April tisa tunatarajia kupokea watalii 300 watatembelea vivutio mbalimbali vya utalii na kundi lingine takribani 600 watawasili April 16″amesema Jaji Mihayo
Mwenyekiti wa bodi hiyo aliongeza kuwa watalii wa ndani wameongezeka kutoka 562 ,549 kwa mwaka 2020 hadi watalii 788,933 kwa mwaka 2021 sawa na ongezeko la asilimia 40.2.
“mapato yanatotokana na utalii wa ndani yameongezeka kutoka sh.bilioni 9.7 kwa mwaka 2020 hadi sh bilioni 12.4 mwaka 2021 sawa na ongezeko la asilimia 27.8″amesema Jaji mihayo
Hata hivyo amesema wawekezaji kutoka taifa la Bulgaria wanatarajia kujenga loji nne k zenye hadhi ya nyota tano zitakazojengwa katika hifadhi za taifa ikiwemo Serengeti,Manyara ,Tarangire na Ngorongoro ambazo zitaendeshwa na Kampuni ya Kempiksi.
Aliendelea kueleza kuwa kupitia filamu Royar Tour imesaidia kuvutia wawekezaji na kuongeza mawakala wa utalii ambapo takribani mawakala 30 wamehamasika kutembelea nchini ili kujifunza na kujionea vivutio mbalimbali na kuvitangaza.
Akitaja ongezeko la watalii nchini Jaji Mihayo alifafanua kuwa mwaka 2015 idadi ya watalii ilikuwa 14,754,mwaka 2016 watalii 22,967 mwaka 2017 watalii 36,640 , mwaka 2018 watalii 31,419 ,mwaka 2019 watalii 16,348 ,mwaka 2020 watalii 6,889 na mwaka 2021 watalii 6,303.
Aidha alimshukuru Rais Samia kwa kuingoza vyema soko la utalii nchini na kuifanya Tanzania kuwa kivutio Cha kwanza Cha utalii Afrika kwa mwaka 2022.
More Stories
Bodaboda wamchangia Rais Samia Mil 1 ya fomu ya Urais
HAYA HAPA MATOKEO YOTE FORM II NA DARASA LA IV
Ufaulu waongezeka matokeo ya Darasa la Nne na Kidato cha Pili